Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Novemba,
2016 amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Bw.
Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera. Uteuzi wa
Bw. Diwani Athuman unaanza mara moja.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa
Bodi katika taasisi tano za Serikali kama ifuatavyo.
Pili,
Rais Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Bw. Sylvester M. Mabumba kuwa Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Uteuzi huu umeanza
tarehe 17 Novemba, 2016.
Tatu,
Rais
Magufuli amemteua Prof. Patrick Makungu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO). Uteuzi huu umeanza
tarehe 16 Novemba, 2016.
Nne,
Rais
Magufuli amemteua Bw. Martin Madekwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia
ya Ardhi. Uteuzi huu umeanza
tarehe 17 Novemba, 2016.
Tano,
Rais
Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI), Uteuzi huu
umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.
0 comments:
Post a Comment