Na Pamela Mollel,Mikumi
Tembo ni
mnyama kubwa kuliko wote lakini sio mrefu kama twiga,kuna aina mbili ya
tembo.tembo w a bara la Afrika na bara
la Asia
Ukitaka
kujua tofauti zao wa bara la Afrika ni wakubwa ,na maskio yao yanamuonekano wa
ramani ya bara la afrika lakini tembo bara la Asia wanamasikio madogo na pia wanaweza kufundishwa kulima na michezo mbalimbali
Akizungumza na waandishi wa habri kuhusu mnyama
huyo (Tembo)Afisa wa shirika la Tanapa katika hifadhi ya Mikumi Abdalla Choma
alisema kuwa Tembo hao wa wa bara la
Afrika wapo katika makundi mawili.
1.Tembo wa msituni wanameno ambayo yamenyooka kwaajili ya kuwawezesha kupita
katika msitu.
2.Tembo wa Savana, meno yao yamepindapinda wanapenda
kuishi katika familia moja wanaweza kuishi kwanzia wawili hadi 45 kwa familia.
Alisema Tembo wauwezo
mkubwa wa kusikia na wanakumbukumbu ya kutosha
Akizungumzia kuhusu uzazi
wa tembo mzee Chuma alisema kuwa tembo wanauwezo wa kubeba mimba na kuzaa kwa
miezi 18-20
Tembo huyo hunyonyesha motto
wake kwa takribani miaka miwili hadi mitatu na motto wa tembo huyo
akishafikisha miaka 15 huesabika ameshakuwa na kutakiwa kuondoka katika familia
hiyo na kwenda kujitegemea
Tembo huishi kwa miaka
60-75 kwa sasa lakini miaka ya nyumba walikuwa na uwezo wa kuishi miaka 80-120
.
“Sababu za kuishi miaka
michache kwa miaka hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi “alisema mzee
Mchoma
CHAKULA CHA TEMBO
Anapenda kula matawi ya
miti na nyasi za chini halafu anakula kwa saa 16 kati ya saa 24.
Kiasi cha chakula
anachokula ni kati ya kilo 150-300 kwa tembo mkubwa na hunywa maji kati ya lita
200 hadi 250.
0 comments:
Post a Comment