Nafasi Ya Matangazo

October 10, 2016




Waziri waViwanda,Biashara na Uwekezaji,Mh.Charles Mwijage (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TBL Group wakati wa hafla ya kutangaza chapa bora 50 za kitanzania katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa  Mlimani City mwishoni mwa wiki.


Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (kulia) na Maofisa wengine wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya  kutangaza na kukabidhi tuzo kwa chapa bora za kitanzania liyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (kushoto) akingalia tuzo za chapa ambazo kampuni yake imejishindia (kulia) ni Meneja wa Chapa ya Konyagi,Martha Bangu,(katikati) ni Meneja wa Chapa ya bia ya Kilimanjaro,Pamela Kikuli.

Wafanyakazi wa TBL Group wakionyesha vyeti vya tuzo ambavyo kampuni imeshinda katika shindano la Chapa bora 50 za kitanzania.

Mameneja wa chapa za TBL Group zilizoshinda wakiwa na wawakilishi wa makampuni mengine.


Makamu wa Rais Mheshimiwa Samiha Hassan Suluhu akimpongeza Aisa wa TBL Group,Edith Bebwa




Meneja wa Chapa ya Bia ya Kilimanjaro ,Pamela Kikuli,akipokea tuzo ya chapa hiyo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage.Wengine pichani ni wajumbe wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo.

Meneja wa Chapa ya Konyagi ,Martha Bangu ,akipokea tuzo ya chapa hiyo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage.Wengine pichani ni wajumbe wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.

Chapa cha vinywaji vya Bia ya Kilimanjaro,Konyagi na Dodoma Wine zinazozalishwa na viwanda vya TBL Group, mwishoni zimetangazwa kuwa chapa bora katika shindano la kuhamasisha watanzania kutumia bidhaa za Tanzania lililoandaliwa na taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)  kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo chapa 50 zimepata tuzo ya ubora.


Hafla ya kutangaza na kutoa tuzo hizo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo mgeni wa heshima alikuwa ni Makamu wa Rais,Mh.Samia Hassan Suluhu pia ilihudhuriwa na viongozi wa taasisi za serikali na watendaji wakuu na wafanyakazi wa makampuni mbalimbali binafsi ambao bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda vyao yalikuwa yameingizwa kwenye shindano

Akihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hafla hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema kuwa kampuni  inajivunia kwa chapa zake  tatu kuweza kushinda na kuwa miongoni mwa chapa bora 50 na kutunukiwa tuzo za ubora.

“Tunazipongeza taasisi hizi ambazo zimeandaa shindano hili la Fahari ya Tanzania kwa kuwa linawezesha wazalishaji wa Tanzania kujikita kwenye uzalishaji wa bidhaa bora za kuweza kushindana kwenye masoko ya hapa nchini na kwenye ngazi ya kimataifa  “.Alisema Jarrin.

Alisema kuwa pia hatua ya kuzinduliwa kampeni ya kuwahamasisha watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ni nzuri kwa kuwa  ikifanikiwa itakuza uchumi wa nchi kwa haraka na kupanua  wigo wa ajira nchini kwa kuwa  mahitaji ya bidhaa yanavyozidi kuongeza kwenye soko ndivyo mapato ya makampuni yanaongezeka na kuiwezesha kuchangia pato kubwa la serikali kwa njia ya kulipa kodi na kuajiri watu wengi zaidi.


“Hizi ni dalili nzuri katika kipindi hiki ambacho serikali imetangaza mkakati wa kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.TBL Group tuaendelea kuunga mkono mkakati huu kwa kuwa tayari tumeishaanza kuutekeleza kwa kuhakikisha uwekezaji wetu unazidi kuleta tija na kuleta mabadiliko kwa jamii.Viwanda vyetu hivi sasa ni tishio kwa kuzalisha bidhaa bora mpaka kwenye ngazi ya kimataifa na vinashikilia rekodi ya kufanya vizuri katika bara la Afrika”.Alisema.

Aliwashukuru wafanyakazi wote wa kampuni hiyo kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha  inazidi kupata mafanikio siku hadi siku “Mafanikio haya yote tunayoendelea kuyapata yanatokana na jitihada za kufanya kazi kwa bidii kwa kila mfanyakazi wa kampuni”.Alisema Roberto.

TBL Group mbali na baadhi ya chapa zake kuingia katika chapa bora 50 nchini  (Top 50 Tanzanian Brands 2016) pia inashikilia tuzo mbalimbali baadhi zake zikiwa ni Tuzo ya Mzalishaji Bora,Tuzo ya Mwajiri bora, na Tuzo ya Mlipa Kodi Bora.
Posted by MROKI On Monday, October 10, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo