Nafasi Ya Matangazo

October 04, 2016



KUFUATIA kitendo cha askari namba  F. 3016 SGT Talib Hamad Kassim ambaye tayari amefukuzwa kazi na Jeshi la Polisi kwa kitendo chake cha kuomba na kupokea  rushwa kutoka kwa raia wa kigeni mjini Zanzibar, Jeshi la Polisi nchini linalaani vikali tabia hiyo na kwamba ni tabia ya askari binafsi na siyo maadili ya askari wa Jeshi la Polisi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi,Kamishna Msaidizi wa Polisi, Advera Bulimba, Kutokana na kitendo hicho, tayari Jeshi la Polisi limemfukuza kazi askari huyo na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria. Aidha, Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya askari wake yeyote atakayekiuka maadili yake ya kazi.

Jeshi la Polisi nchini halitamuonea muhali askari yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya kazi na kutenda vitendo binafsi vinavyo lifedhehesha au kulitia dosari Jeshi la Polisi.
Posted by MROKI On Tuesday, October 04, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo