Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2016

 Baadhi ya vijana wakijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi –NEC (Kulia) waliokuwa wakitoa Elimu ya Mpiga Kura wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana mkoani, wilayani Bariadi, Simiyu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea kutoa Elimu ya Mpiga kura nchini kwa kukutana na wananchi wa makundi mbalimbali.
 Afisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Hubert Kiata akitoa elimu ya Mpiga kura kwa wakazi wa wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
 Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Bariadi waliojitokeza kupata Elimu ya Mpiga Kura iliyokuwa ikitolewa na Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mkoani Simiyu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha programu endelevu za kuwafikia wananchi moja kwa moja kuwapatia elimu ya mpiga kura kupitia mikutano, maonesho mbalimbali na vyombo vya habari.
Maofisa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Hurbert Kiata (kulia) na Upendo wakisikiliza kwa makini Hoja na maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na vijana wa wilaya ya Bariadi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Taratibu na Sheria zinazosimia Chaguzi za Tanzania. Picha / Aron Msigwa –NEC.
Posted by MROKI On Thursday, October 13, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo