Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kabla
ya kuzindua kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akiweka jiwe la uzinduzi
katika kiwanda cha kusindika Maziwa wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akipewa maelezo na
vijana wa kikundi cha Meatu Milk wanaojishughulisha na usindikaji wa maziwa
kabla ya kuweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa Meatu.
: Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde
akizungumza na Vijana na wananchi wa Meatu baada ya Waziri Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama kufungua kiwanda cha maziwa Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana na wananchi wa Meatu wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha maziwa
Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi ya
maziwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua kiwanda
cha maziwa Meatu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Meatu Mhe. Pius Machungwa akipokea zawadi ya maziwa kutoka kwa Waziri Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama mara baada ya kufungua kiwanda cha maziwa Meatu. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Baadhi ya viongozi wa Wilaya Meatu, mkoa
wa Simiyu na viongozi wa kitaifa wakicheza muziki ishara ya kufurahia uzinduzi
wa Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (waliokaa) wa nne) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu, na Vijana wa Meatu Milk.
**********
Na Stella Kalinga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amefungua kiwanda cha
kusindika maziwa kinachoendeshwa na kikundi cha Vijana wa Meatu kilichopo wilayani
humo Mkoa wa Simiyu.
Akizungumza na Vijana hao wanaosindika maziwa ya
Meatu (MEATU MILK), Waziri Mhagama amewataka kuutunza mradi huo ili uwe mradi
mkubwa wa kuwaingizia mapato wao na Serikali kwa ujumla.
Mhagama amesema kwa kadri mradi huo utakavyokuwa
mkubwa ndivyo wafugaji wa Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla
watakavyonufaika kwa kupata soko la uhakika la maziwa.
Aidha, Waziri huyo amewataka Viongozi wote wa wilaya
kuunga mkono juhudi zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
za kuwatengenezea vijana mazingira
mazuri ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo yao, ikiwa ni pamoja na
kushughulikia upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Wakati huo huo Waziri Mhagama ameahidi kuwa Ofisi yake itatoa mkopo wa shilingi
30,000,000 kwa lengo la kuwasaidia vijana hao kuongeza uzalishaji ili kupanua
soko la maziwa yao ndani na nje ya Mkoa.
“Mhe. Mkuu wa Mkoa Ofisi ya Waziri Mkuu itawapa
mkopo vijana wa “Meatu Milk”ili wapanue uzalishaji; Wizara yangu itatoa mikopo
kwa vijana walio tayari kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo
vidogo vitakavyowasaidia kuwapa ajira na kujikwamua kwenye umaskini” alisema
Mhagama.
Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Meatu kabla ya
kumkaribisha Waziri Mhagama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema
Mkoa huo umejipanga kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kutumia malighafi zinazopatikana
hapa nchini.
“Tumejichagua kuwa pacha wa Mhe. Rais katika
kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Vitendo na tumedhamiria kuwa
miongoni mwa mikoa mitano inayofanya vizuri katika uchumi”, alisema Mtaka.
Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa Mhe. Waziri, kiongozi wa kikundi cha Meatu
Milk Lightness Benedicto amesema Halmashauri imewapa mtaji na kuwajengea uwezo
kwenye teknolojia za usindikaji, ufungishaji wa bidhaa za maziwa pamoja na
elimu ya ujasiriamali.
Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Mbuzi ameahidi kuwaongezea
mtaji wa shilingi 5,000,000 vijana hao pamoja na kuwasaidia kukutafuta soko la
uhakika kwa maziwa watakayosindika.
0 comments:
Post a Comment