Nafasi Ya Matangazo

September 26, 2016

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, akizungumza jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea michango ya fedha na vifaa kutoka kwa wanachama wa jumuia hiyo kwa ajili ya walioathirika kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.  Jumla walichanga fedha na vifaa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 60.7.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mtaa Muhonda, Kariakoo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Philimon Chonde, fedha taslimi mchango kutoka kwa wafanyabioashara hao kwa ajili ya walioathirika  kwa tetemeko Kagera. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa JWK, Abdalah Mwinyi na Mweka Hazina wa jumuia hiyo, Silvanus Mande.
 Katibu wa JWK, Mtaa wa Raha Square, Frank Nduta akikabidhi vitenge na bidhaa nyingine kwa Mwenyekiti wa JWK, Philimon Chonde
 Wafanyabiashara wa Mtaa wa Mchikichi Kariakoo, wakitoa msaada wa  misumari kwa ajili ya waathirika wa tetemeke, Kagera.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Posted by MROKI On Monday, September 26, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo