Nafasi Ya Matangazo

September 29, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Mwele Malecela, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Septemba 29,2016 kuhusu Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo na kongamano la 30 linalaotaraji kufanyika kuanzia Oktoba 4-6 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Mwele Malecela, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Septemba 29,2016 kuhusu Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo na kongamano la 30 linalaotaraji kufanyika kuanzia Oktoba 4-6 jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti, Dk Julius Massaga.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Mwele Malecela, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Septemba 29,2016 kuhusu Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo na kongamano la 30 linalaotaraji kufanyika kuanzia Oktoba 4-6 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Mwele Malecela, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Septemba 29,2016 kuhusu Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo na kongamano la 30 linalaotaraji kufanyika kuanzia Oktoba 4-6 jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti, Dk Julius Massaga.
Baadhi ya Wanahabari na Wanasayansi watafiti kutoka NIMR, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Mwele Malecela, akizungumzia Mkutano Mkuu wa Taasisi hiyo na kongamano la 30 linalaotaraji kufanyika kuanzia Oktoba 4-6 jijini Dar es Salaam. 
*************
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeandaa Kongamano lake la 30 litakalo fanyika kuanzia Oktoba 4-6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo litafanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa wa mwaka wa NIMR linataraji kufunguliwa Oktoba 4 na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na litafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya NIMR, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Mwele Malecela alisema kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Uwekezaji katika tafiti zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia.”

Dk Mwele amesema kuwa jumla ya mada 220 zitawasilishwa na kujadiliwa katika Kongamano hilo la Siku 3 ambalo litashirikisha wanasayansi watafiti kutoka nchi mbalimbali duniani.

Alisema kuwa mada hizo zitakuwa katika maeneo mbalimbali ambayo ni Mkakati wa kuboresha afya ya uzazi ya mama, watoto wachanga na vijana, Magonjwa sugu yasiyoambukiza na changamoto zake, Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria, Usalama wa Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi, Mkakati wa afya moja katika kudhibiti magonjwa ya milipuko na Magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.




Mwele aliyeambatana na Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti ambaye pia ni Mtafiti Mkuu wa NIMR, Dk Julius Massaga alisema kuwa mada hizo zinalenga katika kujadili haja ya kuwekeza katika tafiti za mifumo ya utoaji huduma, magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza na tabia na shughuli za kibinadamu zinazochangia kuwepo kwa maradhi.

Mikakati ya kufikia Malengo Endelevu ya Dunia itajadiliwa na mapendekezo kuwasilishwa kwa Serikali na wadau wengine.

“NIMR inaamini kwamba watafiti wana michango mkubwa katika kuleta maendeleo kupitia matokeo ya tafiti mbalimbali wanazofanya juu ya magonjwa ya binadamu. Ni kwa msingi huo basi, Taasisi inasisitiza kwamba kila mtafiti ana jukumu la kuwasaidia Watanzania kufikia malengo endelevu ya dunia kwa kuepuka magonjwa,”alisema Dk Mwele.

Aidha pamoja na uwasilishwaji na majadiliano katika mada mbalimbali, NIMR imeandaa maonesho ya bidhaa zitokanazo na tafiti, taarifa za kitafiti, machapisho, vifaa vya utafiti, nyenzo za kutoa huduma za afya.

Pia kutakuwa na Mikutano maalum miwili itakayojadili Wanawake katika Sayansi na Mikakati ya kuhamasisha ufadhili wa Tafiti kwa Wadau wa ndani ya nchi.

Pia Dk Mwele alisema kutakuwepo na tuzo kwa wanasayansi katika katika makundi mbalimbali ikiwepo  Mtafiti Bora wa Afya Afrika, Mtafiti Bora wa Afya Tanzania, Mtafiti Mbunifu wa Mwaka na Mtafiti Bora katika kuchapisha Maandiko ya Kitafiti.

Mbali na tuzo hizo pia NIMR itamzawadia Kiongozi Mashuhuri wa Tanzania aliyetoa mchango mkubwa katika kuinua na kuimarisha tafiti za afya nchini.

Dk Mwele alisema kuwa jumla ya washiriki 300 wamejisajili kuhudhuria kongamano hilo ambapo washiriki wanatoka katika nchi za Afrika Kusini, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Australia, Denmark, Ubeljiji, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Uswis, Kanada, Sweden, Norway, Marekani, Bangladesh, Thailand na wenyeji wa Tanzania.

Taasisi za Tanzania zitakazo shiriki ni pamoja na Taasisi ya Afya Ifakara, Vyuo Vikuu vya Tiba na Sayansi za Afya vya Muhimbili na Bugando, Chuo Kikuu cha KCMC, Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kilimanjaro, Chuo Kikuu Dodoma, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia, Hospitali ya Rufaa KCMC, AMREF Health Africa, Hospitali ya Rufaa Amana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga.

Dk Mwele alisema kongamano hilo ni wazi kwa watanzania wote kuhudhuria ili kupata taarifa za uhakika kuhusu tafiti za afya zinazofanywa na Taasisi zao.

Aidha alishukuru Makampuni mbalimbali na taasisi za fedha, wafanyabiashara ambao wamedhamini kongamano hilo.
Posted by MROKI On Thursday, September 29, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo