Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Geprge simbachawene akisikiliza maelezo
kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF Bw. Sebera Fulgence kuhusu Mfuko wa
Fidia kwa Wanyakazi (WCF) alipotembelea banda la Mfukohuo, pembezoni mwa
mkutano mkuu wa mwaka wa ALAT mjini Musoma
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umetoa elimu kuhusu mambo mbalimbali
yanayohusu Mfuko kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu 32 na Tuzo za viongozi wa Serikali
za Mitaa (Mayors Award), mjini Musoma mkoani Mara.
Mkutano
huo ulioanza Septemba 22 na kufunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI),
George Simbachawene Septemba 23, 2016, unatarajiwa kumalizika Septemba 24,
2016.
Akitoa
mada kwenye Mkutano huo juu ya shughuli na huduma zitolewazo na WCF, Meneja Uhusiano
Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, (pichani juu), alisema, Mfuko umeanza kutoa Fidia kwa
Wafanyakazi tangu Julai mwaka huu wa 2016 na kuwahimiza waajiri kupeleka
michango yao kama ambavyo Sheria iliyoanzisha Mfuko huo inavyoelekeza.
Wajumbe
wamepata uelewa na madhumuni ya uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,
majukumu yake, jinsi ya kuchangia na viwango vinavyotakiwa kwa mwaka wa fedha
2015/2016 na 2016/2017.
Pamoja
na mambo mengine wamepata fursa ya kupata taarifa kwamba kupitia Tangazo la
Serikali Na 212A la tarehe 30 Juni 2016, Mfuko umeanza kupokea madai na kulipa
mafao kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263
marejeo yam waka 2015] ikisomwa pamoja na Kanuni za Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi za Mwaka 2016
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Bw. Sebera juu ya kazi za Mfuko huo
Maafisa wa WCF wakiwa kwenye banda la Mfuko huo pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa mwaka wa ALAT. Kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, Athumani Khalfan na Zaria Mmanga, wakisubiwri kutoa elimu kwa wajumbe kuhusukaziza Mfuko
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Bw. Sebera juu ya kazi za Mfuko huo
0 comments:
Post a Comment