Nafasi Ya Matangazo

July 22, 2016

Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Tabata mwaka huu Miss Tabata 2016 linafanyika leo  Ijumaa kwenye Ukumbi wa Da West Park, Tabata jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa jumla ya warembo 16 wanatarajia kupanda jukwaani kuwania taji hilo linaloshikiliwa na Ambasia Mallya, ambaye alishinda taji hilo mwaka 2014.

Mratibu huyo aliwataja warembo watakaoshiriki kuwa ni pamoja na Happiness Paul (21), Neema Makwaia (21), Rose Lucas (22), Mariam Maabadi 23), Sabrina Khalifa (20), Catherine Alex (22) na Grace Malikita (21).

Warembo wengine ni Rachel George (21), Nasra Munna (23), Jackline Evarest (21), Flora Msigwa (21),  Noela Pastory (21), Neema Zablon (24) na Jesca Jackson (22).

Aliongeza kuwa warembo watano watakaofanya vizuri katika shindano hilo, watapata tiketi ya kuiwakilisha Tabata katika shindano la Kanda ya Ilala baadaye mwaka huu.

Alisema kuwa warembo watakaoingia tano bora kila moja atazawadiwa kusoma nafasi ya kusoma kozi yoyote katika Chuo cha DataStar Training College. Kila kozi itagharimu 1.8m/-

Mshindi wa kwanza pia atapata fedha  taslimu Sh. 300,000 wakati mshindi wa pili ataondoka na Sh. 200,000 huku mrembo atakayeshika nafasi ya tatu atajinyakulia Sh. 150,000 . 

Mshindi wa nne na watano kila mmoja atapata Sh. 100,000 huku kifuta jasho cha Sh. 50,000 kila m Wengine ni Rachel George (21), Nasra Munna (23), Jackline Evarest (21), Flora Msigwa (21),  Noela Pastory (21), Neema Zablon (24),  Narcisa Wilbert (19) na Jesca Jackson (22).
moja kitatolewa kwa waliobakia.

Bendi ya Twanga Pepeta itatumbuiza kwenye shindano hilo linaloandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment.

Nae Mkurugenzi wa Miss Tabata ambae pia ni mkuu wa kambi Godfrey Kalinga alisema jana kuwa maandalizi ya shindano limekamilika.

Miss Tabata inadhaminiwa na Lete Raha, DataStar College, Global Publishers, CXC Africa, Fredito Entertainment, Yono Auction Mart, Saluti5, Kitwe General Traders na Bob Entertainment
Posted by MROKI On Friday, July 22, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo