Nafasi Ya Matangazo

July 20, 2016

 
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala ( watatu kushoto) akimsikiliza Wakaa wa Vipimo Wilayani humo, Laurent Kabikiye (aliyeshikilia mzani) wakati wa uhakiki wa mizani hiyo.
 
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (mwenye koti kushoto) amewaonya wanunuzi wa Pamba Wilayani humo kuchezea mizani wanazopimia zao hilo wakati wa ununuzi kwa wakulima kwa lengo a kuwapunja wakulima na kujinufaisha zaidi.

Kanali Ndagala aliyasema hayo leo wakati akizindua msimu mpya wa ununuzi wa Pamba alioufanya katika Kijiji cha Kanyonza na kusema kuwa wafanya biashara wahakikishe kuwa mizani wanayotumia haijachezewa kwa namna yeyote na iwe imefanyiwa ukaguzi na wakala wa vipimo.
“Leo tunazindua ununuzi wa zao la Pamba katika maeneo yetu, lakini nitoe angalizo kwa wanunuzi kuhusiana na mizani mtakayoitumia kununulia Pamba isiwe imechezewa na kuwapunja wakulima,”alisema Kanali Ndagala.

Aidha Kanali Ndagala aliwatahadharisha wakulima kuhakikisha pamba wanayoileta sokoni ni Pamba safi na siyo iliyo wekwa maji au vitu vingine vyotote kama mchanga kwa lengo la kuongeza uzito na kujipatia manufaa.

Kanali Ndagala alisema kitendo cha kuweka maji au vitu vingine katika Pamba ni kuharibu bidhaa hiyo na kuharibu soko kwa ujumla la zao a pambamba na kutawafanya wanunuzi kusitisha ununuzi huo katika maeneo yao.
Posted by MROKI On Wednesday, July 20, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo