Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel (kushoto) na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakiosha gari.
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini.
Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akizungumza na baadhi ya wabunge na wageni mbalim bali kuelezea lengo la kampeni hizo asubuhi njini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun wakiosha moja ya magari yaliofika kuoshwa kwa ajili ya harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini.
Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kulia) akimkabidhi fedha za kuoshewa gari Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel.
Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kushoto) wakijitolea kuosha magari kwenye kampeni hizo.
Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na mpiga picha wa magazeti ya The Guardian Ltd, Halima Kambi wakiosha moja ya gari katika kampeni hizo.
Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akishiriki zoezi la kuosha magari.
Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto akishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ Dodoma leo.
Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) wakishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ Dodoma leo.
0 comments:
Post a Comment