Nafasi Ya Matangazo

June 15, 2016

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na mmoja wa wamiliki wa viwanda vidogo vya kukoboa mpunga ambazo zilifungiwa na Jiji na kusababisha ajira za watu zaidi ya 2000 kupotea.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiwasikiliza vijana wanaofanya kazi katika mashine hizo.
 Amos Makalla (kushoto) akizungumza na waelimishaji wa SIDO kutoka nchini Australia.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametengua amri ya kuvifungia viwanda vidogo 28 vya kukoboa mpunga eneo la Sido iliyotolewa na jiji la Mbeya kupitia idara ya mazingira sababu ya kuvifungia viwanda hivyo zikielezwa kuwa ni mlundikano wa pumba katika maeneo hayo.

Uamuzi wa kutengua amri hiyo ametoa leo kwenye ziara ya kutembelea ofisi ya SIDO  Mkoa na kisha kutembelea karakana ya sido, viwanda vidogo vya usindikaji na ukamuaji mafuta ya alizeti na viwanda vya kukoboa mipunga eneo la sido na hapo ndipo alipokutana na umati wa wananchi wakiomba msaada wake kwakuwa viwanda hivyo vimebeba ajira ya watu zaidi ya 2000.

Baada ya kuwasikiliza wananchi hao alitangaza kutengua amri hiyo kwa kuwa kuvifunga viwanda hivyo kutafanya mchele kuadimika na bei itapanda na si jambo jema hasa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu.

Pili ametengua amri hiyo ikizingatia kuna ajira zaidi ya watu 2000 . "Kwa amri hii ya kufunga ukoboaji hivi Hawa watu 2000 wanakwenda wapi? Kama si kurudi mtaani na kwa vijana ni hatari. Hii kauli ya hapa kazi tu kwa Hawa watu 2000 wataifanyia wapi?"

Ameagiza Mkuu wa wilaya, jiji , jumuiya ya wakoboaji washirikiane na uongozi wa Mbeya cement ambao ndiyo watumiaji wa pumba hizo kuongeza uwezo wa kusomba pumba hizo.

Akiwa eneo la Sido magari ya Mbeya cement yaliendelea kusomba pumba na wamemuhaidi Mkuu wa mkoa ndani ya wiki mbili pumba zote zitakuwa zimesombwa.
Posted by MROKI On Wednesday, June 15, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo