Wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja katika mafunzo yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro hivi karibuni na kuwahusisha wenye mabaa na mameneja wao
Wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja katika mafunzo yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro hivi karibuni na kuwahusisha wenye mabaa na mameneja wao
MPANGO wa kuendeleza
wafanyabiashara wadogo wanaouza bidhaa za kampuni ya TBL Group ujulikanao
kitaalamu kama Retail Development Programme umewanufaisha ambapo idadi yao hivi
sasa wanaendesha biashara zao kwa ufanisi na kuboresha maisha ya familia zao na
jamii kwa ujumla.
Katika mafunzo yaliyotolewa
chini ya mpango huu nchini kote baadhi ya wafanyabiashara wamepatiwa elimu
kuhusiana na usimamizi wa fedha binafsi unaolenga kumwezesha
mfanyabiashara kutofautisha fedha zake na biashara ili kuepusha hasara au kufilisika,
mbinu za biashara ikiwa ni pamoja na rasilimali watu na masoko. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Vipengele vingine
walivyofundishwa ni uendeshaji wa biashara ya bia zinazoambatana na matangazo,
kumvutia mteja kwa kuweka mazingira rafiki kwa wateja na uuzaji wa kuwajibika
unaozingatia sheria za vileo, usafi na mazingira ya afya.
Wakiongea kwa nyakati tofauti
kuhusiana na mpango huu baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mafunzo kutoka
mikoa mbalimbali nchini kwa niaba ya wenzao walisema kuwa ni mzuri
na umewawezesha kupata maarifa na mbinu za kibiashara.
Samwel Tarimo mfanyabiashara
wa Mwanza akiongea kwa niaba ya wenzake waliohudhuria mafunzo hayo alisema kuwa
unasaidia kuwawezesha kujua mbinu za kuleta mafanikio katika
biashara wanayofanya na kupiga hatua ya maendeleo
“Elimu inasaidia kujua mambo
mengi na kuleta mabadiliko kwenye jamii na wafanyabiashara tuliohudhuria
mafunzo wengi wetu tumebadilika kuanzia kibiashara mpaka kimaisha
kwa kuwa kuna mambo mengi ambayo alikuwa yanatukwamisha kibiashara hasa
utunzaji wa mahesabu na kufanya mipango ya kibiashara ambayo baada ya kuyajua
mafanikio ameanza kupatikana.
Naye Jane mfanyabiashara
anayeuza vinywaji mkoani Arusha amesema mafunzo yalitotolewa kupitia mpango huu
yamewajengea uwezo wa kujiamini katika biashara wanazofanya “Huu mpango ni
mzuri na unapaswa kuigwa na makampuni mbalimbali kwa kuwa elimu
tuliyopatiwa na TBL imetufumbua macho kwa mambo mengi na
wanaofuatilia masuala waliyofundishwa hivi sasa wanakwenda vizuri kibiashara.
Monica Nyaki, mfanyabiashara
wa vinywaji mjini Moshi alisema licha ya kuwa na muda kwenye biashara yake
lakini mafunzo hayo yamempa mbinu mpya za kujenga mahusiano mazuri na TBL,
wateja na nidhamu ya pesa na usafi maeneo ya kazi na aliongeza kuwa mafanikio
katika biashara yananufaisha familia nzima ya mfanyabiashara na jamii kwa
ujumla.
Mkufunzi wa mafunzo hayo,
Nyakahinja Manyama, alisema hivi karibuni kuwa mafunzo haya yalioendeshwa chini
ya mradi wa Endelea na TBL ambao umelenga kuwawezesha wafanyabiashara wa
vinywaji kujua mbinu za biashara za kuwawezesha kupata mafanikio ikiwemo
kuwezesha kampuni kujenga uhusiano wa karibu na wadau wakiwemo wanaosambaza
vinywaji vyake.
Pia alisema mafunzo haya ni
utekelezaji wa moja ya lengo la kampuni la “kujenga dunia yenye nuru njema
lenye dhamira kuongeza kasi ya ukuaji na maendeleo kwenye jamii.
"Mradi huu wa kutoa elimu
ya biashara kwa wafanyabiashara wa vinywaji umeanza kuonesha mafanikio makubwa
kutokana na mwitikio wa wanaohitaji mafunzo haya kuwa wengi nchi nzima na
tutahakikisha tunawafikia na kuwapatia elimu hii itakayowawezesha kupata
mafanikio katika biashara zao,"alisema.
0 comments:
Post a Comment