Afisa mkuu wa biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya “Bila Salio Wala MB” iliyozinduliwa jana katika hafla iliyofanyika ofisi za makao makuu ya Airtel, ambapo wateja wa Airtel wanapata huduma ya Facebook, Messenger na huduma nyingine zinazopatikana kwenye facebook bure kabisa.
**************
AIRTEL Tanzania, kwa kushirikiana na Facebook, imezindua huduma ya Bure
ya Facebook kwa wateja wa Airtel katika kampeni mpya ijulikanayo kwa
jina la "Bila Salio Wala MB".
Lengo la mpango huu ni kuunganisha kila Mtanzania katika intaneti na, kwa njia hii, kutawezesha kufungua fursa
nyingi ambazo hapo awali zimekuwa ngumu kwao kuzitimiza.
Kama sehemu ya "Bila Salio
Wala MB" kampeni, Watanzania wenye kadi ya simu ya Airtel na simu yenye
uwezo wa kupokea intaneti wataweza kufurahia Facebook, Messenger na huduma
nyingine zinazopatikana kwenye facebook. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa huduma hiyo, Afisa mkuu wa biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty
alisema, "kutokana na maisha ya sasa jinsi yalivyo intaneti ni kitu muhimu
sana katika maisha ya watu kwani imekuwa ikileta maendeleo katika Jamii na
uchumi duniani kote.
Lengo letu ni kuunganisha watu wengi itakavyowezekana na intaneti na kuwatambulisha katika fursa mbalimbali
zilizopo kwa kukuza uchumi wao . Tunaamini kabisa huduma hizi za bure za
facebook ni hatua ya kwanza nzuri ya kufikia lengo hili. "
Free Basics ni seti ya
Kiswahili na tovuti ya kimataifa
Tanzania inayotoa Habari za afya, elimu,
biashara na habari za fedha husiana na
watu ili waweze kufanya uamuzi na maamuzi ya kuboresha maisha yao.
Free Basics ni maarufu sana katika mitandao ya kijamii
duniani kote , inayowawezesha wateja kuwasiliana kwa urahisi na ndugu jamaa na
marafiki zao.
Kuwawezesha wateja wetu kuweza kupata huduma hii bila gharama yoyote , inatoa fursa kubwa kwa mamilioni ya watu ,
urahisi zaidi wa kuwasiliana na pia kuweza kutangaza bidhaa mbali mbali na
hivyo kuweza kujiongezea kipato huku wakitumia mtandao huo wa facebook kwa
kibiashara zaidi ya mawasiliano pekee na kukuza uwezo wao kutokana na utajiri
wa habari wanazoweza kupata kupitia mtandao.
Akitoa maelezo, mkuu wa kitengo
cha intaneti Gaurav Dhingra alielezea "utumiaji wake ni rahisi. Popote
ulipo Tanzania, ilimradi unakadi ya simu ya Airtel iliyosajiliwa katika simu yako yenye uwezo wa kupata intaneti
, unaweza kuingia kwenye akaunti yako ya Facebook, na kufurahia kabisa, huduma
hiyo bila ya kuwa na salio au kifurushi cha intaneti.
Kwa wale ambao sio watumiaji wa Facebook wanaweza pia kuomba njia fupi
ya kuunda akaunti zao kwa kupiga *148*88 #, "aliongeza Dhingra.
0 comments:
Post a Comment