Nafasi Ya Matangazo

June 07, 2016

Meneja wa Bia ya Castle Light Nicholous John, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, baada ya Uzinduzi wa Chupa mpya yenye Ujazo wa milimita 440 iliyofanyika katika Ukumbi wa Break Point Kinondoni Makaburini.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia TBL, Kushila Thomas, akimpa zawadi mmoja wa wananchi walioshiriki katika uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya TBL, wakiwa katika hali ya furaha baada ya uzinduzi wa Bia ya Castle Light yenye ujazo wa milimita 440. --- Kampuni ya bia ya TBL imezindua chupa mpya ya bia yake pendwa aina ya Castle LITE yenye ujazo wa mili lita 440 kwenye uzinduzi uliofanyika baa ya Break Point iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

Kufuatia uzinduzi huu, bia ya Castle LITE yenye ujazo wa mili lita 440 itaanza kupatikana nchi nzima mnamo tarehe 5, mwezi huu. 

Aidha, ladha ya bia ya Castle LITE itabaki na ladha na sifa zile zile za kipekee kama ilivyo kwenye bia hii yenye ujazo wa mili lita 375, hivyo kuweza kunywewa na kuburudisha wakati wowote. 

Akizungumzia uzinduzi huu, Meneja wa bia ya Castle LITE, Nicholous John amesema; “Castle LITE inaendelea kuja na ubunifu mbalimbali kwenye soko la Tanzania, mfano mzuri ni kampeni yetu ya jinsi ya kutumia nembo yenye rangi ya bluu iliyopo kwenye chupa ya Castle LITE kujua kama bia imepata ubaridi stahiki utakaokupa ladha halisi ya Castle LITE. Na sasa tumekuja na Castle LITE yenye ujazo wa mili lita 440 ili kuwapa wateja wetu uwezo wa kuchagua.”

 Castle LITE hii yenye ujazo wa mili lita 440 itauzwa kwa shilingi 2,500 kwa chupa na shilingi 50,000 kwa kreti na itapatikana kote Tanzania. Castle LITE inabaki kuwa bia pekee sokoni yenye nembo ya kipekee inayobadilika rangi na kuwa bluu pale bia inapopata ubaridi stahiki unaomwezesha mnywaji kufurahia ladha ya kipekee ya bia hii. 

Uzinduzi wa Castle LITE yenye ujazo wa mili lita 440 uliambatana na utambulisho wa basi la kipekee lenye majokofu yanayotoa ubaridi wa hali ya juu ya kutunzia na kuuza bia za Castle LITE zenye ubaridi stahiki unaomwezesha mnywaji kufurahia ladha halisi ya ubaridi wa barafu ya Castle LITE.
Posted by MROKI On Tuesday, June 07, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo