Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi, Stella
Kahwa (kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu madhara ya ufungashaji batili wa mazao (LUMBESA) katika maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani ambayo huadhimishw akila
mwaka ifikapo Mei 20,
MKuu wa Kitengo cha Sheria Wakili Mosses Mbunda akijibu maswali
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Sheria ya Ufungashaj iwa Bidhaa
MADA:
YATAMBUE MADHARA YA UFUNGASHAJI BATILI ILI UYAEPUKE NA KUKUZA UCHUMI WA NCHI
A. UTANGULIZI
Ndugu waandishi wa
habari;
Wakala wa Vipimo ni Taasisi
ya Serikali inayosimamia vipimo vyote vitumikavyo ki-biashara Tanzania (Bara) kwa kuhakikisha vinakuwa
sahihi. Pia Kuhakikisha kuwa bidhaa zote
zilizofungashwa zinafungashwa kwa usahihi.
Ili
kuhakikisha kuwa wananchi wanafanya biashara au wanafungasha bidhaa zao kwa
kutumia vipimo sahihi, Maafisa Vipimo katika kila mkoa hufanya ukaguzi kuhakikisha kwamba vipimo
vyote vinavyotumika au ufungashaji wa bidhaa unaofanywa ni sahihi kwa mujibu wa Sheria ya
Vipimo Sura 340 (mapitio ya mwaka 2002).
Tanzania
kupitia Wakala wa Vipimo ni mwanachama
wa Shirika la vipimo Duniani (OIML), hivyo
kila mwaka ifikapo Mei 20
huungana nchi zingine na mashirika mengine Duniani katika kuadhimisha
Siku ya Vipimo. Kauli mbiu ya mwaka huu
(2016) ni ‘Measurements in a Dynamic
World’ BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Kutokana na agizo la
Mh. Waziri Mkuu alilolitoa tarehe 23/3/2016 lililoagiza Wakala wa Vipimo Kuhakikisha inasimamia na kuhakikisha
ufungashaji batili ( Lumbesa) unatokomezwa.
Wakala wa Vipimo
inashirikiana na Taasisi zingine za serikali, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala,
Wakuu wa Wilaya, Halmashauri za miji, vyombo vya usalama n.k. ili kuhakikisha
azma inafanikiwa.
Baada ya utangulizi huo, Wakala wa
Vipimo inapenda kuwafahamisha kuwa baada ya kutolewa elimu kuhusiana na
ufungashaji kwa mtindo wa Lumbesa kwa
sasa tumeanza zoezi maalum la kuzuia uuzaji/ufungashaji
wa mazao kwa mtindo huo.
Ufungashaji
batili ni nini?
Ufungashaji batili
ni ufungashaji kinyume na Sheria ya Vipimo Sura 340 Mapitio ya Mwaka 2002
pamoja na Kanuni zake.
Lumbesa ni nini?
Lumbesa ni ufungashaji batili wa bidhaa ndani ya
kifungashio kwa uzito zaidi ya ule unaokubalika Kisheria au kwa kuunganisha
kifungashio.
Mazao yanatakiwa yauzwe kwa kutumia vipimo sahihi ( wapime
kwenye mizani na siyo kwa kufanya makadirio).
Baadhi
ya Matokeo ya Ufungashaji Lumbesa
- Kumpunja mkulima
- Halmashauri kukusanya mapato pungufu
- Kuathiri afya na maisha ya wabebaji
- Kuathiri nguvu kazi ya Taifa
- Kusababisha migongano katika jamii
Sheria inasemaji kwa
wafungashaji wasiotumia vipimo sahihi
Mtu yeyote atakaye
fungasha, uza, safirisha, au kuonyesha bidhaa kwa nia ya kuziuza zilizofungashwa
kinyume cha Sheria ya Vipimo Sura 340 Mapitio ya Mwaka 2002 na Kanuni zake,
atakuwa ametenda kosa la jinai na ataadhibiwa kwa mujibu wa Sheria.
Matokeo ya zoezi
maalum tangu 4 April – Mei 18/2016
Katika
kusimamia ufungashaji sahihi wa mazao Wakala wa Vipimo inafanya zoezi maalum la
ukaguzi wa ufungashaji batili wa mazao (lumbesa) na tangu tarehe 4 Aprili hadi Mei 18/ 2016, wakosaji
1172 walififilishwa na kulipa faini ya takriban Tshs.123m ikiwa ni adhabu ya
kutokufungasha kwa usahihi.
|
|
WITO
WETU
Wakala wa Vipimo inasisitiza matumizi ya vipimo
sahihi na ufungashaji sahihi katika Biashara.
Aidha, maagizo aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri Mkuu
Bungeni jana, tarehe 19 Juni, 2016, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa
papo; ambapo aliwaagiza Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutumia Kamati
za ulinzi na Usalama na Watendaji Kata na Vijiji kuhakikisha wanapambana na
Wafanyabiashara wenye kujihusisha na ufungashaji huo batili imezidi kutilia
mkazo suala hili.
Hivyo,
tunaahidi kuongeza juhudi na maarifa katika kuhakikisha suala la lumbesa
linakuwa historia hapa nchini.
|
0 comments:
Post a Comment