Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa
Arusha Lengay Ole Sabaya akitoa tamko kwa waandishi wa habari jana jijini
Arusha,ambapo amemtaja Mathias Manga na washirika wake kuwa ni tatizo kubwa
ndani ya chama na kwamba kama akiendelea kuwepo ni Dhahiri kuwa anaweza
kukisambaratisha chama hicho kutokana na kugawa makundi kwa vijana wa chama
hicho kutokana na fedha zake.(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Katibu Hamasa Mkoa wa Arusha Lucas Msomi akisisitiza jambo katika kikao na
waandishi wa habari.
******************
Baraza la vijana mkoa wa
Arusha la chama cha mapinduzi uvccm limetangaza kumvua ukamanda wa vijana
wilaya ya Arumeru bw,Mathias Manga kutokana na kukiujumu chama kwa muda mrefu
hali ambayo imekuwa ikididimiza jitihada za kurejesha imani ya chama hicho.
Bw,Manga ambaye ni
mafanyabiashara maarufu wa madini Mkoani Arusha amekuwa akituhumiwa kwa muda
mrefu kuwa namhausiano ya karibu ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa
Edward Lowassa na kusahau kufanya majukumu ya kichama ambayo yamempa uongozi wa
Ukamanda wa vijana wilaya.
Akitoa maelezo ya tamko
hilo mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengay Ole Sabaya amemtaja Mathias
Manga na washirika wake kuwa ni tatizo kubwa ndani ya chama na kwamba kama
akiendelea kuwepo ni Dhahiri kuwa anaweza kukisambaratisha chama hicho kutokana
na kugawa makundi kwa vijana wa chama hicho kutokana na fedha zake.
Aliongeza kuwa kutokana na
kumvua ukamanda kamanda huyo UVCCM Mkoani hapa haitakuwa tayari kushiriki kikao
chochote cha kamati ya siasa ambapo Manga atashiriki kama mjumbe katika kikao
hicho.
"Sitashiriki kwa namna yeyote
na vijana wangu kwenye kikao cha kamati ya siasa Mkoa ama kikao kingine ambacho
kitanikutanisha na Mathias Manga na nawataka wanachama wa chama cha mapinduzi
kuona kama ni halali kwa huyu aliyeitwa kamanda wa vijana kuendelea kushikilia
kadi yao,"alisema Ole Sabaya
Akitoa onyo kwa
makamanda wilaya ya Arusha mjini,Longido na Monduli kujipima na kujitathimini
kabla ya kufikia uamuzi kama bado wanafaa kuendelea na hadhi ya ukamanda wa
wilaya ama laa,na wakijiona hawatoshi tunawashauri wakae pembeni mapema kabla
ya kutumbuliwa jipu.
Baraza linakiomba
chama cha Mapinduzi kupitia tathini ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana wale wote
walioshiriki kukihujumu chama kuanzia ngazi ya matawi,kata,wilaya na Mkoa washughulikiwe
kwa mujibu wa taratibu za kimaadili kabla ya uchaguzi wa chama 2017 vinginevyo
wakiachwa watashiriki tena kufanya uhasi dhidi ya chama sanjari na kupandikiza
mamluki.
Hata hivyo
mwenyekiti huyo ametengua uteuzi wa wajumbe watano wa baraza katika nafasi za
kuteuliwa ilidumu toka mwaka 2012 na kuunda kamati mpya chini ya mwenyekiti
Lengai Ole Sabaya huku akiwataka viongozi wa chama hicho kumuunga mkono
Rais JohnPombe Magufuli kwa jitihada zake za kupeperusha bendera ya chama na
kufanya kazi kwa uadilifu na kubeba kauli ya HAPA KAZI TU.
0 comments:
Post a Comment