Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri
mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakisali katika kanisa la Bikira Maria
Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amesali ibada ya jumapili ya
pili ya Pasaka tangu kuchaguliwa kuwa Rais.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida
Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na Rais Dkt. John
Magufuli wakifatilia kwa makini mahubiri yaliyokuwa yakitolewa katika kanisa la
Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Kikundi
cha Kwaya ya vijana wakiimba katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato
mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga pamoja na Mke wa Raila Bi. Ida
Odinga wakifatilia kwa makini mahubiri ya Paroko Padre Henry Mulinganisa katika ibada ya pili
ya pasaka Chato Mkoani Geita. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti takatifu kutoka kwa Paroko wa Parokia
ya Bikira Maria Chato Padre Henry Mulinganisa .
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia
ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amechangia kiasi cha Shilingi milioni
10 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato
mkoani Geita.
Waziri
Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira
Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga, Mke wa Raila Bi. Ida Odinga
pamoja na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakishukuru mara baada ya ibada.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sista Maria Theleza Ntihabose wa
kanisa la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
0 comments:
Post a Comment