Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2016


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) jana limefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga ambapo mgeni Rasmi alikua ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza.

Katika hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo, Mahiza aliushukuru uongozi wa TFF nchini kwa kuweza kuandaa mkutano mkuu mzuri na wa kisasa ambao pia ulifanyikia katika mkoa wake wa Tanga.

Akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu, Mahiza alisema, TFF ina changamoto ambazo inapaswa kuzifanyia kazi kwa na hasa katika kuendeleza soka la wanawake nchini ambalo bado mwamko wake uko chini sana.
Mahiza alisema, Mpira wa miguu kwa sasa ni ajira nzuri ambayo inasaidia kujikwamua kiuchumi kwa wachezaji pamoja na familia zao, nayaomba makamouni yajitokeze kuwekeza katika mpira wa miguu na hasa katika soka la wanawake.
“Mahitaji ya wanawake katika kushiriki/kucheza mpira wa miguu ni makubwa zaidi, tofauti na wanaume hivyo kuangalia jinsi gani wadhamini wanapatikana ili kuweza kuwasaidia wanawake” alisema Mahiza.
Mkutano ulijadili Ajenda za kawaida ambazo ni Kufungua Mkutano ni Uhakiki wa Wajumbe, Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita, Yatokanayo na Mkutano uliopita, Hotuba ya Rais, Taarifa kutoka kwa Wanachama, Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.

Zingine ni Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013, Kuthibitisha ripoti ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu, Kupitisha bajeti ya 2015, Marekebisho ya Katiba, Mengineyo na Kufunga Mkutano.

Baada ya majadiliano ya kina mkutano mkuu pia uliazimia kuahirisha ajenda ya marekebisho ya Katiba hadi Mkutano Mkuu ujao utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huuu.
Wakati huo huo Leo Jumapili asubuhi Mkuu wa Mkoa Tanga, Mwantumu Mahiza ameweka jiwe la msingi katika eneo la kituo cha michezo cha kukuzia vipaji lilipo eneo la Mikanjuni jijini Tanga.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi, Mahiza alisema wamejisikia faraja mkoa wa Tanga kupata nafasi hiyo kuwa mkoa wa kwanza kupata kituo cha kukuzia vipaji nchini.

Mahiza alisema uongozi wa Serikali mkoa wa Tanga utashirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA)/TFF katika kusaidia usimamizi wa uendeshaji wa kituo hicho.
Mahiza ameishukuru TFF kwa kuamua kuwekeza katika ujezi wa kituo hicho, ambacho baaade kitatoa nafasi kwa vijana kupata ajira kupitia mpira na shughuli nyingine za maendeleo ya kiuchumi ikiwemo utalii na watu kupata ajira katika kituo hicho.
Posted by MROKI On Sunday, March 13, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo