Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2016

Kikosi  cha Mbeya City Fc tayari kipo jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya African Sports  unaotajia kuchezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mapema leo mkuu wa kitengo cha utabibu kikosi Dr Joshua Kaseko amesibitisha kuwa  wachezaji wote 18 walisafiri kutoka jijini Mbeya tayari wa mchezo huo wako kwenye hali nzuri kabisa na ana imani kubwa watacheza kwenye kiwango bora  ili kuipatia matokeo timu yao hapo kesho.

“Joseph Mahundi alipata majeraha  kwenye mchezo uliopita, hivi sasa yuko vizuri na tunatarajia  atakuwa sehemu ya kikosi  hapo kesho, hakuna shaka kuwa  City iko hapa Tanga  kwa sababu ya kupata matokeo na  hakuna  jambo lingine, tumetoka  kushinda dhidi ya Stand  United  jambo linalotupa nguvu ya kupambana hapo kesho, tuna morali ya hali ya juu kikosini  ambapo kila mmoja  ana  hamu ya kurudi na pointi tatu” alisema.

Kwa upande wake  Kocha Kinnah Phiri ameweka wazi kuwa japo hali ya hewa ya hapa ni tofauti kabisa na ile iliyopo jijini Mbeya lakini hiyo siyo sababu ya City kukosa ushindi hapo kesho


“Hali ya hewa ya hapa ni tofauti sana na iliyopo jijini Mbeya, hilo hatulitizami sana, tumejiandaa vya kutosha, asubuhi ya leo tumemaliza mazoezi na wachezaji wamepewa muda wa kuweka miili yao sawa kwa kwenye barafu, hakuna shaka yeyote kuwa  tunazo pointi tatu kutoka hapa” alisema.
Posted by MROKI On Sunday, March 13, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo