Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja ya vifaa vya hospitali kutoka kwa
wawailishi wa makampini ya Vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam
Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala
ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto
Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha,Wapili kushoto ni Reginald Mengi
ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Wapili kulia ni Basil
Gadzios wa Coca cola Kwanza.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana baadhi ya viongozi vya makampuni
ya vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC
katika makabidhino ya vofaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi
bilioni 10 yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini
Dar es salaam Februari 25, 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Pepsi,
Avinash Jha, Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na
Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya
hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za
vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola- SBC katika
makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini
Dar es salaam Februari 25, 2016. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki.
*********************
SERIKALI imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye
thamani ya sh bilioni 10 kutoka kwa umoja wa kampuni za utengenezaji wa
vinywaji baridi nchini.
Msaada huo wa kwanza kutolewa nchini na makampuni
matatu wapijnzani wakuu katika biashara, Coca Cola, Pepsi na Azam ulipokelewa
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika bohari ya dawa (MSD) Ubungo, Dar es
Salaam jana.
Akipokea Msaada huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
alisema kuwa msaada huo ni mkubwa na waaina yake na umekuja wakati muafaka
wakati serikali ipo katika jitihada za kuboresha huduma za afya nchini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“Msaada huu ni mkubwa sana kuwahi kutolewa nchini,
na umekuja wakati muafaka ambapo Serikali ina fanya jitihada za kuboresha
huduma za afya nchini,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Mbali na msaada huo lakini kampuni hizo kupitia
Kampuni ya Coca Cola italeta watalaam kwaajili ya kutoa mafunzo kwa watalaamu
wa afya katika kuwajengea uwezo kwaajili ya kuvifanyia vifaa hivyo na
matengenezo.
Alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada
kubwa na kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha sekta ya Afya inaboreshwa katika
maeneo ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya
kutolea huduma za afya.
Majaliwa alisema kuwa hivi karibuni Rais Dk John
Magufuli alihamasisha maboresho ya Hopitali ya Rufaa Muhimbili na hasa Wodi ya
wazazi na hatua hiyo ya kupokea msaada wa vifaa ni sehemu ya kumuunga mkono
Rais katika jitihada hizo.
Majaliwa alisema licha ya uhasimu wa kampuni hizi
katika soko la bidhaa zao lakini wamekaa pamoja na kuamua kuunga mkono jitihada
za Rais John Magufuli katika uboreshaji wa huduma za afya nchini.
Alisema kuwa Kampuni hizo tatu kupitia umoja wao
huo zimekabidhi msaada wa vifaa tiba vinavyofanya kazi kwa teknolojia ya kisasa
na vitaweza kutumika katika mazingira yeyote nchini hata Hospitali za rufaa.
Majaliwa alisema kitendo cha kampuni hizo kutoa
msaada huo mkubwa ambao ameupokea ikiwa ni kontena 20 ya futu 40 yenye makasha
1,500 ya vifaa vipya kabisa na vifaa
mbalimbali zaidi ya 300 vikiwemo vitanda 80 na magodoro yake unapaswa
unastahili kupongezwa na kila mtanzania na kuungwa mkono na wadau wengine
katika kunusuru afya za watanzania.
Vifaa hivyo vyote vitasambazwa katika vituo vya
afya, Zahanati, hospitali za wilaya na Mkoa pamoja na Hospitali za rufaa nchini
kote hasa katika maeneo ya pembezoni.
“Vifaa hivi vitawafikia watanzania wote,
vitasambazwa maeneo mengi nchini hasa katika maeneo ya pembozoni ambako
kunakabiliwa na changamoto kubwa ya vifaa tiba,” alisema Majaliwa.
Kuhusu usambazaji wa vifaa hivyo Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa alisema serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD), itahakikisha
vifaa vinasambazwa jkwenda kwenye vituo husika kwa umakini mkubwa ili viweze
kumutumika kama ilivyokusudiwa.
“Tayari tunayo orodha ya awali ambako tunatarajia
kupeleka vifaa hivi katika mikoa ya Dodoma, Geita, Katavi, Kilimanjaro, Kigoma
na Lindi. Mikoa mingine ni Mara, Mbeya, Mtwara, Shinyanga na Tanga lakini pia
mikoa ya tabora na Rukwa, Pwani, Singida na Iringa yote yaweza kupata,” alisema
Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu alitoa pia angaliza kuwa vifaa hivyo
vikatumike kama ilivyo kusudiwa na akitoa onyo kwa watumishi wasio waadilifu
kuwa endapo wataiba vifaa na kwenda kuviuza watakiona cha moto.
Katika upande wa ushirikiano na sekta binafsi
Waziri Mkuu Majaliwa amesema pande hizo mbili zikishirikiana kikamilifu
zitaleta mabadiliko makubwa nay eye kuahidi kwa bniaba ya serikali kuendelea
kuboresha ushirikiano.
Mapwema akizungumza kwa niaba ya Kampuni hizo
tatu, Mkurugenzi Mkuu wa Coco Cola Kwanza, Basil Gadzios alisema licha ya
ushindani na uhasama wao katika soko la bidhaa zao lakini walikaa na kuamua kwa
pamoja jinsi ya kuwasaidia watanzania katika upande wa afya.
“Licha ya ushindani wetu huu katika masoko ya
bidhaa zetu lakini tulipo fikiria afya za watanzania tuliamua kuungana na kukaa
pamoja na kuamua kutoka msaada huu wa vifaa tiba,”alisema Gadzios.
Aidha Gadzios alitoa pongezi kwa Rais Magufuli
katika jitihada zake za kukabiliana na rushwa nchini jambo ambalo alisema
linawatia moyo na kuahidi kuendeleza uwekezaji wao hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurian Bwanakunu alisema
kampuni ya hizo za vinywaji baridi na washirika wao wa Medshare International
wamekuwa mara kwa mara wakitoa msaada mbalimbali nchini kwa MSD.
0 comments:
Post a Comment