Nafasi Ya Matangazo

February 26, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja ya vifaa vya hospitali kutoka kwa wawailishi wa makampini ya Vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha,Wapili kushoto ni Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Wapili kulia ni Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana baadhi ya viongozi vya makampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino ya vofaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi bilioni 10 yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha, Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. 
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola- SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. 
*********************
SERIKALI imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya sh bilioni 10 kutoka kwa umoja wa kampuni za utengenezaji wa vinywaji baridi nchini.

Msaada huo wa kwanza kutolewa nchini na makampuni matatu wapijnzani wakuu katika biashara, Coca Cola, Pepsi na Azam ulipokelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika bohari ya dawa (MSD) Ubungo, Dar es Salaam jana.

Akipokea Msaada huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa msaada huo ni mkubwa na waaina yake na umekuja wakati muafaka wakati serikali ipo katika jitihada za kuboresha huduma za afya nchini.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“Msaada huu ni mkubwa sana kuwahi kutolewa nchini, na umekuja wakati muafaka ambapo Serikali ina fanya jitihada za kuboresha huduma za afya nchini,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Mbali na msaada huo lakini kampuni hizo kupitia Kampuni ya Coca Cola italeta watalaam kwaajili ya kutoa mafunzo kwa watalaamu wa afya katika kuwajengea uwezo kwaajili ya kuvifanyia vifaa hivyo na matengenezo.

Alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada kubwa na kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha sekta ya Afya inaboreshwa katika maeneo ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Majaliwa alisema kuwa hivi karibuni Rais Dk John Magufuli alihamasisha maboresho ya Hopitali ya Rufaa Muhimbili na hasa Wodi ya wazazi na hatua hiyo ya kupokea msaada wa vifaa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais katika jitihada hizo.

Majaliwa alisema licha ya uhasimu wa kampuni hizi katika soko la bidhaa zao lakini wamekaa pamoja na kuamua kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika uboreshaji wa huduma za afya nchini.

Alisema kuwa Kampuni hizo tatu kupitia umoja wao huo zimekabidhi msaada wa vifaa tiba vinavyofanya kazi kwa teknolojia ya kisasa na vitaweza kutumika katika mazingira yeyote nchini hata Hospitali za rufaa.

Majaliwa alisema kitendo cha kampuni hizo kutoa msaada huo mkubwa ambao ameupokea ikiwa ni kontena 20 ya futu 40 yenye makasha 1,500 ya vifaa vipya kabisa  na vifaa mbalimbali zaidi ya 300 vikiwemo vitanda 80 na magodoro yake unapaswa unastahili kupongezwa na kila mtanzania na kuungwa mkono na wadau wengine katika kunusuru afya za watanzania.

Vifaa hivyo vyote vitasambazwa katika vituo vya afya, Zahanati, hospitali za wilaya na Mkoa pamoja na Hospitali za rufaa nchini kote hasa katika maeneo ya pembezoni.

“Vifaa hivi vitawafikia watanzania wote, vitasambazwa maeneo mengi nchini hasa katika maeneo ya pembozoni ambako kunakabiliwa na changamoto kubwa ya vifaa tiba,” alisema Majaliwa.

Kuhusu usambazaji wa vifaa hivyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD), itahakikisha vifaa vinasambazwa jkwenda kwenye vituo husika kwa umakini mkubwa ili viweze kumutumika kama ilivyokusudiwa.

“Tayari tunayo orodha ya awali ambako tunatarajia kupeleka vifaa hivi katika mikoa ya Dodoma, Geita, Katavi, Kilimanjaro, Kigoma na Lindi. Mikoa mingine ni Mara, Mbeya, Mtwara, Shinyanga na Tanga lakini pia mikoa ya tabora na Rukwa, Pwani, Singida na Iringa yote yaweza kupata,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu alitoa pia angaliza kuwa vifaa hivyo vikatumike kama ilivyo kusudiwa na akitoa onyo kwa watumishi wasio waadilifu kuwa endapo wataiba vifaa na kwenda kuviuza watakiona cha moto.

Katika upande wa ushirikiano na sekta binafsi Waziri Mkuu Majaliwa amesema pande hizo mbili zikishirikiana kikamilifu zitaleta mabadiliko makubwa nay eye kuahidi kwa bniaba ya serikali kuendelea kuboresha ushirikiano.

Mapwema akizungumza kwa niaba ya Kampuni hizo tatu, Mkurugenzi Mkuu wa Coco Cola Kwanza, Basil Gadzios alisema licha ya ushindani na uhasama wao katika soko la bidhaa zao lakini walikaa na kuamua kwa pamoja jinsi ya kuwasaidia watanzania katika upande wa afya.

“Licha ya ushindani wetu huu katika masoko ya bidhaa zetu lakini tulipo fikiria afya za watanzania tuliamua kuungana na kukaa pamoja na kuamua kutoka msaada huu wa vifaa tiba,”alisema Gadzios.

Aidha Gadzios alitoa pongezi kwa Rais Magufuli katika jitihada zake za kukabiliana na rushwa nchini jambo ambalo alisema linawatia moyo na kuahidi kuendeleza uwekezaji wao hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurian Bwanakunu alisema kampuni ya hizo za vinywaji baridi na washirika wao wa Medshare International wamekuwa mara kwa mara wakitoa msaada mbalimbali nchini kwa MSD. 
Posted by MROKI On Friday, February 26, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo