Baada ya kufanya semina ya ujasiriamali na kutoa elimu ya kuboresha mtaji kwa vijana takribani vijana 300 mkoani Morogoro, Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel kupitia Mpango wa Airtel Fursa imeendeleza na dhamira yake ya kuboresha maisha ya watanzania na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao.
Kwa
kuthibitisha dhamira Airtel FURSA imemkabidhi mjasiliamali wa bucha
la nyama wa mji mdogo wa Ngerengere, wilayani Morogoro, Hashim
Mikidadi , vifaa vya kisasa vinavyotumika katika kazi yake, jokofu,
pamoja nakukarabati bucha, vyenye jumla ya thamani ya shilingi
milioni tisa.
Hashim
Mikidadi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 aliyejikita katika shughuli za
ujasiliama wakati akiendelea na elimu ya Sekondari ili kukidhi mahitaji ya
shule na chakula pamoja na kusaidia wazazi wake ambao ni wazee. Akiwa Katika
umri wa miaka 17 alianza kuweka akiba ya Ths. 300,000 iliyopatikana kutokana na
kazi ya kufyatua na kuuza matofali. Aliamua kuzitumia pesa hizo na
kuwekeza katika kilimo cha Ufuta ambapo baada ya misimu miwili ya kilimo
, Hashimu alifanikiwa kupata shilingi laki Tsh 800,000 ambazo alianzisha
biashara ya bucha ambayo anaendelea nayo hadi sasa.
Akiongea
kwa furaha mara baada ya kukabithiwa vifaa hivyo Mjasiriamali Mikidadi ,
aliishukuru mungu kwa kupata msaada huu kupitia Airtel Fursa na kusema “
nilianza biashara nikiwa na mtaji mdogo ambao haukidhi mahitaji ya biashara
yangu. Sikuwa na vifaa vya kuniwezesha kufanya biashara yangu kwa ufanisi
lakini leo Airtel kupitia Airtel FURSA imeniwezesha na sasa naamini ntawawezesha
kuendesha biashara hii na kuisadia familia yangu pamoja na jamii
inayonizunguka”
“Napenda kutoa shukrani pia kwa wafanyakazi wa Airtel kwa kushiriki katika
ukarabati mkubwa wa bucha langu kwani uwepo wa vifaa hivi vya
kisasa katika bucha yangu ni kuhamasisha wateja wangu na wale ambao si
wateja wangu wavutiwe kupata huduma kutoka katika hii” alisema
Mikidadi.
Akiongea wakati wa kumkabithi vifaa hivyo, Meneja wa Huduma za
Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema Airtel inaijali jamii inayowazunguka
na kuzielewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana zao ikiwa ni
pamoja na ukosefu wa ajira na ukosefu wa mitaji wa kuanzisha biashara zao
na mpango wa Airtel Fursa ni njia moja wapo ya kubadirisha maisha
yao.
Leo unayofuraha kumpatia msaada wenye thamani ya shilingi
milioni 9 ikiwa vifaa, ni pamoja na gharama za ukarabati mkubwa
uliofanyika kwenye bucha hiyo ambayo kwa sasa imekuwani ya
viwango vya juu katika mji wa Ngeregere .
“Airtel FURSA” ni mradi endelevu unaowalenga vijana
nchi nzima kwa kuwapatia vifaa ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali
kupitia mtandao ili kufikia malengo yao.
Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 ikiwa na
taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya biashara unayoifanya, mahali na namba za
simu. Unaweza pia kutuma maombi yako kwa kupitia barua pepe ya airtelfursa@tz.airtel.com. Or tembelea tovuti yetu ya www.airtel.com na ujaze
fomu yako ya maombi
0 comments:
Post a Comment