Waziri wa nishati na madini, Prof.Sospeter Muhongo amekuwa na vikao na wawekezaji zaidi ya 300 kutoka pande zote za dunia ikiwemo Tanzania ambao wanahitaji kuwekeza katika sekta ya nishati.
Katika kikao cha mwisho kilicho fanyika leo Ferbruari 18,2016 amewaaeleza wawekezaji hao kuwa kwa sasa Serikali inatumia mwezi mmoja tangua kuanza mazungumzo hadi kufukia muafaka wa kumruhusu mwekezaji huo kuwekeza au laa tofauti na ilivyokuwa hapo awali zoezi hilo lilikuwa likitumia miezi sita na zaidi.
Prof. Muhongo amesema watanzania walionesha nia ya kuwekeza kutumia fursa hiyo na kwa wale waliongia ubia na wageni kutoka nje wahahikishe wanatimiza lengo walilolikusudia kwa kuiwezesha Tanzania kupata umeme wa uhakika ili kutimiza azma ya Srikali ya kufikia uchumi wa kati mwaka 2025.
Aidha amewatoa hofu wawekezaji na kuwahidi kuwa Serikali itawaunga mkono kwa kila hatua watakayokuwa wamepia.
0 comments:
Post a Comment