Msemaji
wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko akionyesha kwa waandishi wa habari namba
inayotumika katika kuhakiki taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba kwa
kutumia simu ya mkononi kushoto ni Kamishna Msaidizi Kanda ya Dar es salaam Bw.
Mathew Nhonge.
************
Frank
Mvungi
Serikali
yaanza kutumia mfumo wa simu za mkononi kuwawezesha wamiliki wa ardhi kuhakiki
na kuboresha taarifa zao za ardhi kote nchini.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko
wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutambulisha huduma hiyo
mpya kwa wananchi.
“Mfumo
huu unamwezesha mmiliki wa ardhi kuhakiki na kuboresha taarifa zake za ardhi
kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa kuandika neno Ardhi kwenda namba 15774”
alisisitiza Luandiko
Akifafanua
Luandiko amesema kuwa wakati mwananchi anatuma ujumbe huo anatakiwa awea na
nyaraka zake za umiliki wa ardhi au barua ya toleo kwa wale ambao bado
hawajapata hati.
Akizungumzia
faida za mfumo huo Luandiko amebainisha kuwa utasaidia kulinda milki za wateja
na kuondoa kabisa tatizo la matapeli.
Faida
nyingine ni kuongeza uwazi katika kugawa ardhi na hivyo kupunguza migogoro ya
ardhi ambapo hati milki zitatolewa kwa wingi zaidi kwa kuwa mfumo huo ni rafiki
katika utoaji wa huduma.
Aidha
mfumo huu utarahisisha Mawasiliano kati ya mmiliki wa ardhi na Wizara hali
itakayoongeza tija katika upatikanaji wa huduma kwa kuwa zinaweza kupatikana
kwa njia ya simu ya mkononi ikilinganishwa na hapo awali ambapo mwananchi
alitakiwa kufika katika Ofisi za Wizara ili kupata huduma husika.
0 comments:
Post a Comment