Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimweleza jambo
Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) ofisini kwake
mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
Balozi
wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad, akisaini kitabu cha wageni
kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Balozi
wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad, akielezea uzoefu wa Norway
kwenye sekta ya gesi na mafuta katika kikao chake na Waziriri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Kikao hicho pia kilihusisha
watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mbele katikati)
akiongoza kikao kilichohusisha Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie
Kaarstad aliyeambatana na ujumbe wake, watendaji wa Wizara ya Nishati na
Madini pamoja na taasisi zake. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Naibu
Katibu Mkuu- Nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) na Naibu
Katibu Mkuu- Madini Prof. James Mdoe. (kushoto) wakifuatilia kwa makini
maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie
Kaarstad (hayupo pichani).
Naibu Katibu Mkuu- Nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo akifafanua jambo katika kikao hicho.
****************
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo, ameiomba nchi ya Norway
kuisaidia Tanzania kupitia mafunzo hususan katika utafutaji na uchimbaji
wa gesi na mafuta ili kuongeza wataalam wa gesi na mafuta nchini.
Profesa
Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake na balozi wa Norway Nchini
Hanne-Marie Kaarstad aliyeambatana na ujumbe wake uliomtembelea ofisini
kwake jijini Dar es salaam.
Kikao
hicho pia kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini
ambao ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu- Nishati, Dk. Mhandisi Juliana
Pallangyo, Naibu Katibu Mkuu- Madini Prof. James Mdoe.
Aidha,
kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka katika taasisi zilizopo
chini ya Wizara ambazo ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA)
Profesa
Muhongo alisema kuwa sekta mpya ya utafiti na uchimbaji wa gesi na
mafuta inahitaji wataalam zaidi na kuongeza kuwa serikali imekuwa
ikiwapeleka wataalam wake kwenda kusomea masuala ya gesi na mafuta
katika vyuo vilivyoko nje ya nchi kama Scotland na Uingereza.
Alisema
kuwa serikali imeanzisha kozi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na Chuo cha Madini Dodoma.
“ Bado
tuna uhitaji mkubwa wa wahadhiri wenye Shahada za Uzamifu (PhD) kwa
ajili ya kufundisha katika vyuo vyetu, na kuzalisha wataalam
watakaofanya kazi katika makampuni yanayojishughulisha na utafiti na
uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.
Akielezea
kuhusu hali ya umeme nchini Profesa Muhongo alisema kuwa hali ya umeme
nchini ni nzuri kutokana na serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa
wananchi wanapata umeme wa uhakika.
Alisema
kuwa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imekuwa ikisambaza
nishati ya umeme vijijini pamoja na kutoa ruzuku kwa wazalishaji umeme
mdogo kwa njia ya maji (min-hydro) na kuitaka Norway kuisaidia REA ili
iweze kufanikisha miradi yake.
Akielezea
changamoto katika uzalishaji wa umeme nchini Profesa Muhongo alisema
ipo mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya maji yenye kuhitaji
matengenezo na kuiomba serikali ya Norway kusaidia matengenezo ya
mitambo hiyo.
Aliongeza
changamoto nyingine ni vyanzo vya maji kutosimamiwa ipasavyo katika
mabwawa ya maji ya kuzalishia umeme na kusisitiza kuwa tayari serikali
imeanza kufanyia kazi changamoto hiyo.
Naye
Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad alisema kuwa serikali ya
Norway imekuwa na ushirikiano mzuri na serikali ya Tanzania katika sekta
ya nishati na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.
0 comments:
Post a Comment