Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa nje toka Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
Habari leo jijini Dara es salaam kuhusu
utaratibu mpya wa utoaji wa Huduma kwa wagonjwa wa nje ambapo huduma zitakuwa
zikitolewa kuanzia Jumatatu hadi jumamosi ikiwa ni moja ya mikakati ya
Hosipitali hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi.
Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi Neema
Mwangomo akizungumza leo jijini Dar es salaam
wakati wa mkutano na Vyombo vya habari amabapo aliwataka Watanzania
kutumia huduma zinazotolewa na Hospitali hiyo ya Taifa kwa kuwa inao wataalamu wakutosha kutimiza
jukumu hilo la kuwahudumia wananchi.
Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa nje toka Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano ulioenga kueleza mikakati ya
Hosipitai hiyo katika kuboresha huduma zake kwa wananchi.kushoto ni Afisa
Uhusiano wa Hospitali hiyo Bi Neema Mwangomo na kushoto ni Muuguzi wa Hospitali
hiyo Bi June Samwel. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
*****************
Na. Jovina Bujulu –MAELEZO.
Hospitali ya Taifa Muhimbili
imesema kuwa inaendelea kuboresha huduma za afya ili kupunguza msongamano wa
wagonjwa kupitia utaratibu mpya wa madaktari
Bingwa kuwaona wagonjwa kupitia Kliniki zilizoanzishwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Idara ya Huduma
ya Wagonjwa wa Nje wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akizungumza
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo leo jijini Dar es
salaam amesema kuwa utaratibu huo utawasaidia wagonjwa kupata huduma kwa wakati
na kupunguza muda kusubiri huduma.
Amesema utaratibu huo
utawahusu wagonjwa wote wanakwenda kutibiwa katika Hospitali ya Muhimbili na
kuondoka hususan wale wanaolipa fedha taslimu na wale ambao ni wanachama wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bima za mbalimbali za Afya na watumishi ambao
makampuni yao yana mikataba na Hospitali kutibu wafanyakazi wao.
Dkt. Mwenesano ameeleza
kuwa tayari Kliniki hizo zimekwisha anza kufanya kazi na kuongeza kuwa katika
hatua hiyo madaktari Bingwa pekee ndiyo watakaoona wagonjwa wakati wa siku za
kazi kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni, pia jumamosi kuanzia saa 3
asubuhi hadi za 8 mchana.
“Muhimbili tumeamua
kufanya mabadiliko haya kuanzisha Kliniki na kuwatumia madaktari bingwa peke kwa lengo la kuboresha
huduma zetu, awali tulikuwa na Kliniki hizi lakini huduma zake zilikuwa hazitolewi
kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na kutokuwepo kwa muda wa kutosha wa
mdaktari hao kuhudumia wagonjwa” Amesisitiza.
Aidha, amefafanua kuwa wagonjwa
wanaopatiwa rufaa kuja hospitali ya Muhimbili wataendelea na utaratibu wa kawaida
wa kwenda na Barua za Rufaa ili waweze
kupatiwa huduma.
0 comments:
Post a Comment