Mkurugenzi
wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba, akikata utepe
wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel Express lililopo Kariakoo
mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam, akishuhudia ni wakala mkuu wa Airtel
kutoka Celnet, Bwana Kalpesh Bandar.
Mkurugenzi
wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati),
akiangalia simu aina ya Bravo Z10 wakati wa uzinduzi wa duka jipya la
Airtel Express lililopo kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam. Akitoa
maelezo kuhusu simu hiyo ni Afisa mauzo wa Airtel , Meshack Joseph
(kwanza kulia) , akishuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel, James
Moilo.
Afisa
mauzo wa Airtel , Meshack Joseph (kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu
simu mbalimbali za smartphone zinazopatikana katika duka jipya la Airtel
Express Kariakoo wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya lililopo
Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam. Pichani ni Mkurugenzi wa
kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati) akiwa na
wateja pamoja na wafanyakazi wa Airtel. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Airtel
Tanzania imezindua duka la Airtel Xpress mtaa wa msimbazi, Kariakoo Dar
es Salaam ikiwa ni moja ya mipango yake ya kusogeza huduma zake karibu
zaidi na wateja wake.
**************
Kuzinduliwa
kwa duka la kariakoo Airtel Xpress inaongeza idadi ya maduka kuongezeka
kufatia uzinduzi wa dula jipya la kisasa lililoko Morocco Dar es salaam
ulifanyika wiki iliyopita.
Katika
uzinduzi wa duka la Airtel XPress kariakoo mkuu wa kitengo cha huduma
kwa wateja Airtel Adriana Lyamba alisema, kufunguliwa kwa duka la Airtel
Xpress kariakoo itawawezesha wateja wa Airtel na wafanya biashara wa
Kariakoo, Ilala, Magomeni kupata huduma zetu kwa ukaribu zaidi kama
kujipatia simu za kisasa na kwa bei nafuu. Tunaimani kufunguliwa kwa
duka hili hapa kutatasaidia kupata huduma kwa uharaka na ubora zaidi.
“Airtel
tumejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wetu zaidi ya milioni 10
nchi nzima. Kipaumbele chetu ni kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma
kiurahisi zaidi na kwa ufanisi wakati wote na hili limejidhihirisha leo
kwa kufungua duka la Airtel Xpress”, aliongezea Adriana
Baadhi
ya huduma zitakazotolewa kwenye duka la Kariakoo ni pamoja na Airtel
Money, kusajili laini, huduma za internet na huduma zetu nyinginezo.
Pamoja
na duka jipya lililozinduliwa kariakoo pia Airtel inamaduka sehemu
mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam kama Airtel Morroco, Mlimani
City, J Mall, Buguruni Airtel inatarajia kufungua maduka zaidi ifikapo
Juni 2016 yatakayotoa huduma sambamba na mawakala wake Zaidi ya 80,000
nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment