Nafasi Ya Matangazo

January 04, 2016

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Sellasie Mayunga akikabidhi ofisi mbele ya waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Wizara, Dar es Salaam ambapo amemshauri Naibu Katibu Mkuu mpya Dr. Moses Kusiluka kushughulikia kwa ukaribu suala la mpaka wa Kimataifa wa eneo la Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi kutokana na jambo hilo kuwa na maslahi makubwa ya Taifa.


Pia, amemsahuri Naibu huyo kutoa kipaumbele kwa ujenzi wa kituo cha kupokea picha za anga (Satellite receiving station) kilichopangwa kujengwa nchini mkoani Dodoma ambapo pamoja na faida zingine kitarahisisha utoaji wa hati za hakimiliki za ardhi kimila. 
Posted by MROKI On Monday, January 04, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo