Taarifa ya kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na kaimu meneja uhusiano
wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro (pichani ),
imeeleza kuwa sababu ya kuzimwa kwa mtambo huo, ni kuruhusu mkandarasi
kuunganisha bomba jipya na bomba la zamani katika tanki la Maji
wazo-Tegeta, zoezi ambalo linaashiria kukamilika kwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini, hivyo
kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma
ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na
mtambo wa Ruvu chini.
“Tunaelekea kwenye hatua za mwisho za kupokea Maji mengi kutoka mtambo
wa Ruvu Chini baada ya kazi ya upanuzi inayoelekea kukamilika mapema mwezi
February mwaka huu, na kiasi cha Maji kitaongezeka
kutoka wastani wa Lita Milioni 182,000 zinazozalishwa sasa hadi Lita Milioni
270,000.
Hivyo kuzimwa kwa mtambo huu ni moja ya hatua za mwisho-mwisho katika
ukamilishaji wa Mradi wa Ruvu Chini” alisema Lyaro Kwa mujibu wa taarifa hiyo,
DAWASCO imetoa wito kwa wateja na wananchi wote kuhifadhi Maji ya kutosha na
kuyatumia kwa matumizi muhimu ili kukidhi mahitaji husika kwa kipindi hicho
chote.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa matengenezo hayo yatasababisha maeneo mengi
ya jiji la Dar es salaam kukosa Maji, pamoja na mji wa Bagamoyo vijiji vya Zinga, Kerege na
Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani,
Mbezi Beach na Kawe.
Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza,
Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa
Muhimbili, Buguruni, Chang’ombe na Keko.
0 comments:
Post a Comment