Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaban Mwinnjaka.
*******
Na Father Kidevu Blog
RAIS John Magufuli ameivunja kuanzia leo iliyokuwa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kumsimamisha kazi aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa TPA pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.
RAIS John Magufuli ameivunja kuanzia leo iliyokuwa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kumsimamisha kazi aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa TPA pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.
Mbali na maamuzi hayo ya Rais lakini Pia Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa ametangaza kuwasimamisha
kazi watumishi wa nane na viongozi wa TPA.
Kutokana na utendaji mbovu wa mamlaka ya Bandari
Tanzania kwa muda mrefu na kwa kitendo cha kutochukua hatua kwenye vyanzo Rais
Mgufuli amevunja ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi ya TPA, Prf. Joseph
Msambichaka pamoja na uteuzi wa Mkurugenzi wa TPA, Awadh Massawe.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema wakati wa ziara yake TPA alitoa
maagizo mfumo wa malipo bandarini ubadilike kutoka billing system na uwekwe
mfumo wa e-payment amnbao tayari ulianza kuwekwa uwe umekamilika kufikia
Desemba 11, mwaka huu.
“Kwakuwa ripoti iliwataja waliohusika na
upitishaji wa makontena na hakuna hatua iliyochukuliwa, kuaniz muda huu
nawasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na
utaratibu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Majaliwa aliwataja watu hao kuwa ni Wasimamizi wa
bandari Kavu (ICD) Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi
Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, john Elisane na James Kimwomwa
ambaye alihamishiwa Mwanza.
Aidha aliwataja vipongozi wa sekta zilizotoa
ruhusa ya makontena kutoka ndani ya bandari ambao hawamo kwenye ripoti ila ni
wahusika wakuu kuwa ni pamoja na Aliyekuwa meneja Mapato akahamishiwa makao
Makuu kitengo cha Fedha, Shaban Mngazija, Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu
wa bandari Kavu (ICD) ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi wa
Co-oparate Service , Rajab Mdoe.
Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Ibin Masoud,
Meneja Bandari Msaidizi –Fedha, Apolonia Mosha na James Kimwomwa.
0 comments:
Post a Comment