MFUKO
wa Pensheni wa PPF, umeibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya uwasilishaji bora wa
hesabu zake katika kipindi cha mwaka 2014.
Katika
hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za serikali na za watu binafsi, Bodi ya Taifa
ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu, NBAA, imetoa tuzo hizo kwa makampuni na
taasisi mbalimbali nchini, ambapo kwa upande wa kundi la Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii, PPF ndiyo iliibuka ya kwanza ambapo Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko huo,
Bw. Martin Mmari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. William Erio, alipokea tuzo
hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Khamis
Mwinyimvua. Pichani Bw. Mmari akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Khamisi Mwinyimvua. (Picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
Bw. Khamisi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa kuwasilisha taarifa sahihi za hesabu
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Bw. Martin Mmari, (katikati), akiwa amekamata tuzo wakati wa kupiga picha na
baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko huo kwenye hafla ya kutolewa tuzo ya taasisi iliyowasilisha taarifa za mahesabu za mwaka
2014 kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu kwenye kituo cha mikutano
cha Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu NBAA, huko Bunju nje kidoto ya jiji la
Dar es Salaam, Desemba 5, 2015. PPF ilishika nafasi ya kwanza katika kundi la
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hizo hutolewa na NBAA.
Bw. Mamri (wapili
kulia), akigongesha glasi na mmoja wa waalikwa wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya wawakilishi wa PPF katika hafla hiyo
0 comments:
Post a Comment