Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha(APET) Petro Ahham akimkabidhi
kikombe cha ushindi wa bonanza la amani
na utalii mkoa wa Arusha,nahodha wa timu ya Kitambi Noma, James Lugangira
Wanamichezo wa kitambinoma wakiwa wanashabikia ushindi mara baada ya
kukabidhiwa kombe katika kiwanja cha General Tyre jijini Arusha
Na Woinde Shizza,Arusha
Klabu ya Kitambi noma ya jijini Arusha, juzi ilitwaa ubingwa wa soka katika
tamasha la kwanza la amani na utalii ambalo lilifanyika viwanja vya General
Tyre jijini Arusha.
Timu hiyo ilitwaa ubingwa baada ya kuzishinda timu za Wazee Klabu na
chuo cha Uandishi wa habari Arusha(AJTC) kwa kukusanya alama nyingi kutokana na mashindano yaliyoendeshwa kwa
mfumo wa Ligi.
Katika tamasha hilo, liliandaliwa na taasisi ya Arusha media jumla ya
timu sita zilishiriki katika michezo mbali mbali na sambamba na kutolewa burudani
ya ngoma za asili kutoka kikundi cha
Cultural Arts Center cha chuo kikuu cha Makumira
Hata hivyo kwa upande wa mpira wa pete, timu ya Wazee Qeen ilifanikiwa kutwaa
ubingwa baada ya kuichapa katika mchezo wa fainali timu ya AJTC Qeen magoli
34-7.
Katika mchezo wa kukimbiza kuku, timu ya Kitambi noma ilishinda dhidi
ya Wazee Klabu na kwa upande wa wasichana AJTC ilishinda dhidi ya Wazee Qeen.
Akikabidhi zawadi za washindi , Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha,
Petro Ahham alipongeza timu zote zilizoshiriki kutokana kudumisha amani kwa
vitendo.
"tamasha hili limekuja wakati muafaka kwani Arusha ni jiji la
kitalii ambalo linahitaji amani wakati wote hivyo kufanya michezo kuhimiza
amani na utalii ni jambo jema sana"alisema
Awali Katibu wa chama cha soka wilaya ya Arusha,Zakhayo Mjema
alipongeza taasisi ya Arusha Media kwa kuandaa tamasha hilo la amani na utalii
katika jiji la Arusha.
"matamasha kama haya yalipaswa kufanywa na chama cha soka lakini
tumekwama hivyo, tunapongeza Arusha Media kwa kusaidia kuendeleza michezo
katika jiji la Arusha"alisema.
Tamasha hilo, lilidhaminiwa na Shirika la hifadhi za
taifa(TANAPA),kampuni ya vinywaji ya Cocacola, kampuni ya Sunny Safaris,
kampuni ya Big Expedition na kampuni ya Marera Lodge &tours.
0 comments:
Post a Comment