Nafasi Ya Matangazo

December 02, 2015

Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Vicoba, Saccos na wasindikaji ngozi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye kongamanola uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali na vikundivilivyosajiliwa (Kikoa)

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) Mkoani Manyara,Isaya Shekifu akizungumza jana katika kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro (kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo Mahamoud Kambona na kushoto ni mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani humo Reginald Kileo.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud  Kambona akizungumza wakati akifungua kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima yaafya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo waMirerani, (kushoto) ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa mkoahuo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa Tarafa ya Moipo Joseph Mtataiko. SOMA ZAIDIBOFYA HAPA.


Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa Mkoawa Manyara, Isaya Shekifu akiandika maswali yaliyokuwa yanaulizwa katika kongamano la uhamasishaji wampango wa bima ya afya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mjimdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. 
*************
Na Woinde Shizza
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaasa viongozi wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) kuishinikiza bohari ya dawa nchini (MSD) kutoa dawa zinazohitajika.
Kambona aliyasema hayo jana mji mdogo wa Mirerani kwenye uzinduzi wa kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa (Kikoa).

 Kambona alisema amepata malalamiko kwenye vituo vya afya Mirernai na Orkesumet kuwa wamekuwa wanaomba dawa MSD na kuzilipia lakini wanapatiwa dawa ambazo hawana mahitaji nayo hivyo kupata hasara.
“Haina maana watu waagize dawa za malaria wao wawape dawa za kuvimba miguu zisozohitajika, ila NHIF mpo karibu na watu wa MSD, zungumzeni nao ili watoe dawa zinazoombwa na siyo kwa matakwa yao,” alisema Kambona. 

Pia, alivitaka vikundi vya ushirika wa Saccos, Vicoba, Amcos, Vibindo, wachimba madini, waendesha bodaboda, mama na baba lishe na wasindika ngozi, wajiunge na bima ya afya ya Kikoa ili wapatiwe  atibabu kwa unafuu. 

Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) mkoani Manyara Isaya Shekifu  alisema mpango huo wa kikoa utamwezesha mwanachama wa kikundi kupata matibabu yote kama watumishi wa serikali wanavyopata kwenye zaidi ya vituo 6,000 nchini nzima kwa mchango mtu mmoja sh76,800 wa mwaka.

Shekifu alisema gharama za matibabu nchini zinapanda kila uchao na huwa vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuzimudu pindi anapougua, bali kupitia kikoa wajasiriamali nchini watanufaika kupitia matibabu watakayoyapatiwa.

“Ugonjwa haupigi hodi bali humpata mtu wakati wowote na gharama za matibabu zipo juu, ila kupitia mikoa wajasiriamali watapata matibabu bila tatizo lolote, hivyo wanapaswa kujiunga kwa wingi kwenye bima hii,”alisema.

Mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani Manyara, Reginald Kileo alitaja mafao hayo yatahusisha* *gharama za kujiandikisha kumuona daktari, dawa zote zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, vipimo vidogo na vikubwa kama MRI na CT Scan, kulazwa na miwani ya kusomea.

 “Mafao mengine ni upasuaji mdogo na mkubwa na upasuaji wa kujifungua kwa wanawake, matibabu ya kinywa na meno, matibabu ya macho, mazoezi ya kimatibabu ya viungo (physiotherapy) na vifaa saidizi kama magongo na vishikizi vya shingo,” alisema Kileo.

Posted by MROKI On Wednesday, December 02, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo