Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) imeingia
kambini jana jioni katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es
salaam, kujiandaa na ziara ya mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki
itakayoanza Disemba Mosi mwaka huu.
Kocha wa timu hiyo Sebastian Mkomwa amesema vijana wote wameshawasili
jijini Dar es salaam na leo wameanza mazoezi asubuhi katika uwanja wa
Karume watakapokua wanajifua kila asubuhi na jioni mpaka siku ya safari.
Kikosi cha wachezaji 24 kimeingia kambini kujifua na ziara ya Afrika
Mashariki, ambapo timu hiyo inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki kuwania
kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 17, zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Madagascar.
Timu ya Taifa ya vijana imeakua na program ya kukutana kila mwisho wa
mwezi kwa ajili ya kufanya mazoezi na kucheza michezo ya kirafiki na
timu za kombani za U15 katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo kwe mwezi
Disemba itakua pamoja kwa wiki tatu katika nchi za Afrika Mashariki
ikicheza michezo ya kirafiki.
Disemba Mosi, U-15 itasasiri kuelekea jijini Mwanza ambapo itacheza
mchezo mmoja wa kirafiki na kombani ya jijini Mwanza (U17), kasha
kusafiri kueleka mkoani Kigoma itakapocheza michezo miwili dhidi ya
kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).
Ziara hiyo itaendelea katika jiji la Kigali kwa kucheza michezo
miwili dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda (U17), Jinja dhidi ya timu ya
Taifa ya Uganda (U17), Nairobi dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (U17) na
kumalizia kwa mchezo dhidi ya kombaini ya mkoa wa Arusha (U17) na kurudi
jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment