Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa
na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kucheza mchezo wa
kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya vijana wenye
umri chini ya miaka 23 (Amaglug-glug) Jumanne jioni kwenye dimba la
Eldorado jijini Johannesburg.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya kuwakabili Algeria
Novemba 14 jijini Dar es salaa katika uwanja wa Taifa na marudiano yake
kufanyika Novemba 17 jiji Algiers kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya
Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Taifa Stars iliyokweka kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya
mazoezi kila siku katika uwanja wa Edenvale, baada ya kuwa na mazoezi ya
stamina na pumzi kuweka uwiano sawa wa mazoezi (fitness level), Kocha
wa Stars Charles Mkwasa sasa anaendelea na mazoezi ya kutengeza mfumo
kwa wachezaji wake.
Awali Stars ilikuwa icheze mechi mazoezi kesho Jumapili na timu ya
University of Pretoria inayoshriki ligi kuu ya Afrika Kusni (PSL),
lakini baada ya Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) kuandaa mchezo
dhidi ya U23, sasa mchezo dhidi ya Tucks hautakuwepo.
0 comments:
Post a Comment