Nafasi Ya Matangazo

November 08, 2015

Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa (wa pili kulia)) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Kata ya Mazinde wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel Kanda ya Kaskazini Aluta Kweka.
***************
Katika juhudu zake za kuhakikisha watanzania waishio mjini na vijiji wanapata huduma bora za mawasiliano , kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wa mawasiliano katika kata ya mazinde wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga
Uzinduzi huo wa mnara wa mawasiliano utawahakikishia wakazi wa Mazinde na vijiji vya jirani mawasiliano ya uhakika katika  kuendesha shughuli zao za kijamii na kiuchumi kila siku ikiwemo kilimo cha katani.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa alisema"  tunafurahi kuwa na mnara huu wa mawasiliano kwaajili ya wakazi wa Kata ya Mazinde ambao utasaidia kukuza biashara zao na kuinua utandawazi kupitia simu zao za mkononi"

Aliongeza kwa kusema" mawasiliano ndio chachu ya maendeleo ya uchumi wa jamii na ulimwengu kwa ujumla.  na nimatumaini yetu kuwa huduma hii inayozinduliwa hapa leo itachangia kwa kiasi kikubwa endeshaji wa mashamba ya katani, kilimo, biashara mbalimbali na pia kuchagia katika  kubadilisha maisha ya wengi na kwa hilo tunapenda kuwashukuru sana Airtel "

Kwa upande wake, Meneja mauzo wa kanda ya kaskazini, Aluta kweka amesema kampuni yake iko mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma za mawasiliano za uhakika zitakazorahisisha ukuaji wa uchumi na pato la taifa

" katika ulimwengu wa leo wa sayansi na technologia  watanzania wanatakiwa kuwezesha ili kupata fulsa zitokanazo na huduma bora za mawasiliano.  Tunaamini mnara huu hautawahakikishia wakazi wa hapa mawasiliano ya uhakika tu bali utachangia kwa kiasi kikibwa katika kuongeza pato la taifa kwa ujumla"

Kufatia uzinduzi huo, zaidi ya wakazi takribani  10,000 na vijiji  vitatu  vitafaidika na bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo , huduma za intaneti, Airtel money, yatosha na nyingine nyingi
Posted by MROKI On Sunday, November 08, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo