Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta
wa Kenya akiangalia burudani ya ngoma ya utamaduni mara tu alipowasili uwanja
wa ndege wa kimatiafa wa jomo Kinyetta nchini Kenya leo.
Papa Francis akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta
wa Kenya baada ya kuwasili nchini humo ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku sita kwa nchi za Afrika za Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku Papa akitarajiwa kueneza ujumbe wake wa Amani, maridhiano,
mashauriano na kuchochea juhudi za kuzima migawanyiko.
. Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Margaret Kenyatta na kulia ni Naibu Rais wa Kenya, William Ruto.
Afisa wa mawasiliano wa Vatican Padri Federico
Lombardi alisema kwamba kwa Jorge Mario Bergoglio, ambalo ndilo jina kamili la
Papa Francis, hii itakuwa ziara yake ya kwanza kabisa Afrika.
Hii ni ziara ya 11 ya Francis akiwa kama papa nje
ya Vatican. Mapapa wawili wamewahi kuzuru mataifa haya kabla yake.
HONGERA PAPA
ReplyDelete