Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar
es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi akiongozana na
wahadhiri wa Chuo Kikuu hicho wakielekea kwenye uwanja wa hafla ya mahafali
yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini
Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi (watatu kutoka
kulia) na viongozi wa chuo hicho wakiwa
wamesimama wakati unaimbwa wimbo wa Taifa kabla ya kuanza hafla ya mahafali ya
3 yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana jana ambapo wahitimu
walitunukiwa shahada,stashahada na vyeti katika fani mbalimbali.
***************
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar
es Salaam,Rais Mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hasani Mwinyi amewataka
watanzania kuchangamkia fursa za masomo ya taaluma mbalimbali nanayotolewa na Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo eneo la
Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa mahafali ya tatu ya chuo hicho kwa upande
wa Tanzania jana ambapo wahitimu walitunikiwa shahada ,stashahada na vyeti vya
kufuzu fani mbalimbali alisema chuo
hicho kinatoa elimu bora kwenye fani
mbalimbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa za kujiendeleza ili wapate
maarifa ya kuwawezesha kupambana katika soko la ajira ikiwemo kupata maarifa ya
kuwawezesha kujiajiri kutokana na elimu
watakayokuwa wameipata. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Alipongeza wawekezaji kwenye sekta ya elimu na kuiomba
serikali kushirikiana nao li nchi iweze kupata wataalamu wa kutosha “Napongeza
kwa uwekezaji huu na tunaomba serikali izidi kuunga mkono wawekezaji katika
sekta ya elimu ili Taifa liweze kupata wataalamu wa kutosha.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mohamed Ndaula alisema kuwa chuo kimejipanga
kuendelea kutoa elimu bora kuanzia kwenye miundombinu na walimu waliobobea
katika fani mbalimbali na uzoefu mkubwa wa kufundisha vyuo vikuu sehemu
mbalimbali duniani.
Pia alisema kuwa Chuo hicho kimefanikiwa kupata leseni ya
kujiendesha nchini badala ya kuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu Cha
Kampala kilichopo nchini Uganda.
0 comments:
Post a Comment