Nafasi Ya Matangazo

November 21, 2015

 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi akiongozana na wahadhiri wa Chuo Kikuu hicho wakielekea kwenye uwanja wa hafla ya mahafali yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi (watatu kutoka kulia)  na viongozi wa chuo hicho wakiwa wamesimama wakati unaimbwa wimbo wa Taifa kabla ya kuanza hafla ya mahafali ya 3 yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana jana ambapo wahitimu walitunukiwa shahada,stashahada na vyeti katika fani mbalimbali.
Sehemu wa wanafunzi waliohitimu chuoni hapo jana
***************
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam,Rais Mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hasani Mwinyi amewataka watanzania kuchangamkia fursa za masomo ya taaluma mbalimbali nanayotolewa  na Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa mahafali ya tatu ya chuo hicho kwa upande wa Tanzania jana ambapo wahitimu walitunikiwa shahada ,stashahada na vyeti vya kufuzu fani  mbalimbali alisema chuo hicho kinatoa elimu bora  kwenye fani mbalimbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa za kujiendeleza ili wapate maarifa ya kuwawezesha kupambana katika soko la ajira ikiwemo kupata maarifa ya kuwawezesha kujiajiri kutokana na  elimu watakayokuwa wameipata. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Alipongeza wawekezaji kwenye sekta ya elimu na kuiomba serikali kushirikiana nao li nchi iweze kupata wataalamu wa kutosha “Napongeza kwa uwekezaji huu na tunaomba serikali izidi kuunga mkono wawekezaji katika sekta ya elimu ili Taifa liweze kupata wataalamu wa kutosha.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa  Mohamed Ndaula alisema kuwa chuo kimejipanga kuendelea kutoa elimu bora kuanzia kwenye miundombinu na walimu waliobobea katika fani mbalimbali na uzoefu mkubwa wa kufundisha vyuo vikuu sehemu mbalimbali duniani.

Pia alisema kuwa Chuo hicho kimefanikiwa kupata leseni ya kujiendesha nchini badala ya kuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu Cha Kampala kilichopo nchini Uganda.
Posted by MROKI On Saturday, November 21, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo