Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson
Mmbando pamoja na Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel
wakionyesha huduma mpya ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel
kudownload application na kupata
huduma zote kwa urahisi kupitia simu zao .
************
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua application itakayowawezesha
wateja wake kupata huduma zote za Airtel kwa urahisi na kupitia
application ijulikanayo kama “Airtel
care App”
Application hii mpya ya
“Airtel care App” ni
moja kati ya huduma nyingi za kibunifu zinazotelewa na Airtel zenye
lengo la kuwawezesha wateja wa Airtel kutatua matatizo yao na mahitaji
yao
kwa urahisi wakati wowote
Akizungumza Wakati wa uzinduzi wa “Airtel care App” Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema " Airtel tumejikita katika kutafuta, kujua mahitaji ya wateja wetu kwa lengo la kubuni bidhaa na huduma zinazokidhi na kutatua haja zao wakati wote.
“Airtel care App”
inawawezesha wateja wetu, kuchagua kwa
urahisi na kufanya mambo mengi zaidi katika simu zao ikiwemo kuongeza
salio, kuangalia salio, kuangalia matumizi na kiasi kilichosalia,
kununua vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti, kutuma na kupokea
pesa, kununua mlio wa sauti, kupata ripoti ya miamala ya pesa uliyofanya
pamoja na kupata msaada kwa watoa huduma. Huduma zote hizi zinapatikana
kupitia application hiyo ya
“Airtel care App”bila gharama yoyote ya ziada.
Ili kupata “Airtel care App” mteja anaweza kupakua au kudownload Kupitia Google Play kwa simu aina ya Android na kwa simu Iphone wanaweza kupata huduma hii kwa kupakua au kudownload application kwenye Apple store.
0 comments:
Post a Comment