Nafasi Ya Matangazo

October 02, 2015

Mzunguko wa raundi ya sita ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) unatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi na Jumapili kwa timu 10 kucheza kusaka alama 3 muhimu. 

Jijini Tanga Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani, Majimaji FC watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Jumapili Stand United chama la wana watawakaribisha watoza ushuru wa jiji la Mbeya (Mbeya City) katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na Toto Africa watakua wenyeji wa JKT Ruvu jijini Mwanza uwanja wa CCM Kirumba.

Ligi Daraja la Kwanza nchini (Star Times First League) inaendelea wikiendi hii kwa makundi yote matatu kucheza, michezo 11 itachezwa mwishoni mwa wiki siku za Jumamos na Jumapili katika viwanja mbalimbali nchini.

Jumamosi Kundi A, Ashanti United watakua wenyeji wa Mji Mkuu (CDA) katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, KMC watawakaribisha Polisi Dodoma katika uwanja wa Mabatini – Mlandizi.

Kundi B, Lipuli FC watawakaribisha Polisi Morogoro katika uwanja wa Wambi mkoani Iringa, Kimondo FC watakuwa wenyeji wa JKT Mlale kwenye uwanja wa CCM Vwava – Mbozi, huku Burkinafaso ya Morogoro ikiwakaribisha Njombe Mji katika uwanja wa Jamhuri.

Kundi C, JKT Kanembwa watakuwa wenyeji wa Panone FC katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, JKT Oljoro watawakaribisha Polisi Moro uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Geita Gold watacheza na Rhino Rangers uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita na Polisi Tabora watawakaribsiha Mbao FC mjini Tabora uwanja wa Ali Hassa Mwinyi.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo miwili ya Kundi A, Friends Rangers watacheza dhidi ya African Lyon uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, na Polisi Dar watakua wenyeji wa Kiluvya FC katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Posted by MROKI On Friday, October 02, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo