Timu ya Taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) imedhibitisha
kushiriki michuano ya timu za Taifa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA Chalenjji) itakayofanyika nchini Ethiopia kuanzia Novemba 21 –
06 Disemba, 2015.
Michuano ya CECAFA Chalenji ndio michuano mikongwe zaidi barani
Afrika ambapo jumla ya nchi 12 wanachama hushirki michuano hiyo
iliyofanyika mara ya mwisho mwaka juzi nchini Kenya na wenyeji kutwaa
Ubingwa huo.
Nchi wanachama wa CECAFA ni Tanzania Bara, Kenya, Uganda, Burundi,
Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somali, Sudan, Sudan Kusini na
Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa
na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo mchana katika
uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo dhdi ya Malawi utakaocheza Jumatano
Oktoba 7, 2015 kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018
nchini Urusi.
Stars inayonolewa na kocha mkuu mzawa Charles Mkwasa, akisaidiwa na
Hemed Morroco, Peter Manyika na mshauri wa Ufundi Abdallah Kibadeni
wameingia kambini jana katika hoteli ya Urban Rose iliyopo Kisutu jijini
Dar es salaam.
Wachezaji wote wameripoti kambini isipokuwa wachezaji wa kimataifa
wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa, Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu wanaotarajiwa kuungana na wenzao mwishoni mwa wiki
baada ya kumaliza michezo inayowakabili wikiendi hii.
Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa All Mustafa, Aishi Manula,
Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Haji
Mwinyi, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub
“Cannavaro”.
Wengine ni viungo Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Said
Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva, Farid Musa,
washambuliaji John Bocco, Rashid Mandawa na Ibrahim Hajibu
0 comments:
Post a Comment