Kaimu
Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bwana Michael
Mhando akizungumza na wafanyabiashara wa wasamaki katika Soko la
feri hawapo pichani juu ya vikundi vya wajasiliamali wadogo na
wakubwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bwana Michael
Mhando akimkabidhi kadi ya uanachama ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) Mvuvi wa Samaki wa Soko Kuu la Feri Bwana Mohamed Ally
Masoud mwishoni mwa wiki Jijini Dara es Salaam.
Afisa
Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Grace Michael
akotowa eli kwa wavuvi jinsi ya na kujiunga na mfuko huo04.Mkurugenzi
wa Mfuko wa Afya ya Jamii Eugen Mikongoti akimffanulia jambo Mvuvi wa
samko katika soko Kuu la samaki Fer leo jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiendelea kueli misha leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka.
***************
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF leo umekabidhi bima ya Afya kwa Wavi
wadogowadogo (UWAWADA) wa mkoa wa Dar es Salaam,na Kaimu Mkurugenzi wa
mfuko huo,Michael Mhando .
Mhando
amekabidhi Bima hizo leo kwenye soko kuu la kuuzia samaki Jijini Dar es
Salaam maarufu ‘soko la feri’ ambapo awali ua kukabidhi bima hizo
alisema kuwa anawapongeza wanachama wote wa uwawada waliojikusanya kwa
vikundi vya watu kumi na kuhitaji siku ya leo kukabidhiwa Bima zao za
NHIF kwa wanachama 10 waliojiunga na mfuko huo.
Alisema
wanachama hao baada ya kukaa na kusikiliza huduma zinazotolewa na
shirika hilo, namna ambavyo wamefanikiwa kufikia hatua hiyo ya
kukabidhiwa bima zao kupitia mpango wa KIKOA ambao unawalenga hasa
wajasiliamali wadogowadogo.
Aidha
alisema kuwa vikundi husika kujiunga na mfuko huo ,hunufaika na mafao
ya matibabu sawa na wanachama wanaochangia kupitia mishahara yao ya
kila mwezi.
Mhando
alisisitiza kuwa lengo kubwa la mpango wa Mfuko wa Taifa wa Biama ya
Afya ni kuyafikia makundi yote ya wajasiliamali wadogo na wakubwa ili
kuwajumuisha katika mpango huo.
”Lengo
letu kubwa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kuyafikia makundi yote
ya wajasiliamali wadogo na wakubwa ili kuweza kuwajumuisha katika mpango
huu”alisema Mhando.
0 comments:
Post a Comment