Tume ya Taifa
ya Uchaguzi imepokea jumla ya rufaa 54
za madiwani kupinga Maamuzi ya
Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini. Pia jumla ya rufaa 198 za madiwani kutoka Halmashauri
mbalimbali.
Tume
imeanzakupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Wagombea (warufani) na Wasimamizi
wa Uchaguzi kutoka majimboni. Imeanza kuzitolewa maamuzi rufaa za Wabunge. Leo tarehe 31/82015 zimejadiliwa na kuamuliwa
rufaa 38.
Zilizobaki mawasiliano yanaendelea kati ya Tume na Wasimamizi wa
Uchaguzi ili kupata vielelezo vinavyohusika kuisaidia Tume kufikia maamuzi ya
kisheria na haki kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki katika uchaguzi.
Wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa na Wasimamizi wa Uchaguzi ni 16
na Tume imerudisha wagombea 13 kati ya
hao, waliobaki ni 3 ambao Tume imeridhia maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi. Hii
ni kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa kutoonesha makosa ya kisheria au
kiufundi.
0 comments:
Post a Comment