Mkuu wa Biashara wa Fastjet Lan Petrie (kulia), akizungumza katika semina hiyo.
Meneja Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (kulia), akizungumza katika semina ya siku moja ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, iliyohusu kuongezeka kwa safari za ndege za shirika hilo kila siku kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Ofisa Mtendaji wa Masula ya Biashara wa Fastjet, David Chacha, akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari katika semina hiyo.
Ofisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro akizungumza kwenye semina hiyo.
Hapa semina ikiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya
wateja Fastjet, Kampuni ya ndege ya Kiafrika yenye gharama
nafuu imeongeza safari zake za kimataifa kutoka Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwenda Johanessburg Afrika Kusini.
Safari hizo ambazo hivi sasa zitafanyika kila
siku zimepangwa kwa kuwapa abiria fursa zaidi na njia mwafaka na
mbadala kwa nauli wanayoimudu.
Utaratibu huo mpya wa safari za
Johannesburg utaanza kufanya Oktoba Mosi, 2015 na tiketi kwa ajili ya
safari tayari zimeshaanza kuuzwa, ambapo nauli hizo
zinaanzia kiwango cha chini cha dola za Marekani 50 kwa safari ya
njia moja, bila kujumuisha gharama za uwanja na tozo za serikali.
Akitangaza safari hizo mpya Meneja Mkuu wa
Fastjet Kanda ya Afrika Mashariki tawi la Tanzania Jimmy Kibati alisema kwamba
kuongezeka kwa safari kupo sambamba na sera za kampuni hiyo za
mwitiko kwa mahitaji ya wateja.
“Kila mara tunaahidi kuongeza kuongeza masafa
kwenye safari zetu na hasa wateja wanapozihitaji,” alisema Kibati akibainisha
kwamba kuongezeka kwa masafa kumesisitizia jukumu la
Fastjet Tanzania kukua kwenye mtandao wake kikanda, kuufanya usafiri wa
anga kuwa rahisi, salama pia waumudu.
Kibati aliongeza kusema
kuwa kuongezeka kwa utaratibu huo pia kumetoa
uwezekano wa kuingiza ndege ya ziada kwenye
usafiri wa Tanzania baadaye mwezi huu na
hivyo kufanya idadi ya ndege A319 kufikia nne.
“Ukweli tunafurahi kwa mapokeo haya chanya
ambayo Fastjet imeshayapata ndani ya Tanzania na kwa nchi jirani ambako
inafanya safari zake,” alisema Kibati.
“Kwa kutumia gharama nafuu, Fastjet
zinaifanya usafiri wa anga kufikiw akwa urahisi kuliko ilivyokuwa
awali, ambapo abiria wetu wengi wanakuwa wasafairi wa kwanza ambao
kama sio hivyo wasingeweza kusafiri kwa njia ya anga,” alisema Kibati.
Utaratibu huu mpya
unafuatia kutangazwa hivi karibuni uendeshaji ambapo
ilitangaza kuwa na idadei kubwa ya abiria kwa mwenzi.
Katika kipindi cha Julai, Fastjet
ilisafirisha jumla ya abiria 71,763 ikiwa ni ongezeko la
asilimia 36 ikilinganishwa na kipindi cha Julai mwaka jana. Jumla ya mzigo
uliosafirishwa kwa mwezi Julai ulikuwa ni sawa na asilimia 72
na kiwango cha kuwahi kilikuwa cha juu kwa asilimia 95 ya kuwasili kwa muda
unaotakiwa.
Njia ya Johanessburg ambayo
inajumuisha Harare, Zimbabwe na Lusaka Zambai hivi sasa zitawapa
wateja wake njia mbadala ya ziada kwa kusafiri kwa urahisi kwenda na
kurudi kwenye maeneo yao.
Fastjet pia imeongeza mara mbili masafa yake
kwenye njia mpya iliyozsinduliwa hivi karibuni ya Dar es Salaam -
Lilongwe kutoka safari mbili hadi nne kwa wiki, ambayo
imefuatiwa sio muda mrefu tangu kuanza kwa safari zake kati ya miji
hiyo miwili Julai 29, 2015. Njia ya Dar es Salaam
na Kilimanjaro kwenda Entebbe zinabakia kuwa ni safari tatu kwa wiki.
Tiketi unaweza kufanywa kwa njia ya
mtandao kupitia tovuti ya www.fastjet.com, kupitia ofisi za fastjet kwa saa
24 au kupiga simu namba +255 784 108 900, na malipo yanaweza
kufanyika kwa fedha taslim au kupitia kwenye mitandao ya simu ya Mpesa na
Tigopesa.
0 comments:
Post a Comment