Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty akitoa neno la shukrani baada ya
kupokea msaada wa madawati na vifaa vya elimu kwa ajili ya shule ya msingi
Mbuyuni kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar
Trust,wengine pichani wa kwanza kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi
Mbuyuni Dorothy Malecela,katikati ni Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Hassan Maajar
Trust Bi.Zena Tenga na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa
Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akimfundisha mtoto kusoma
akiwa kwenye moja ya chumba chenye madawati yaliyotolewa kwa shule ya msingi
Mbuyuni na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust,
(kulia) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford
Bw.Oliver Mutere.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kulia) na Mkurugenzi wa
Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere (kushoto) wakikata utepe kuashirikia ufunguzi
wa moja ya darasa la shule ya Msingi wa Mbuyuni lililowekewa madawati mapya
ambayo yametolewa kwa shule hiyo na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia
taasisi ya Hassan Maajar Trust.
Walimu wa
shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa
ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya
Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa
madawati.
Wanafunzi
wanaosoma katika shule ya awali katika shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika
picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni
ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya
kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.
****************
Watoto wa shule ya awali ya
Mbuyuni iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wamenufaika na msaada
wa madawati kutoka kwa kampuni ya Matangazo na Mawasiliano ya
Aggrey&Clifford yenye thamani ya shilingi milioni 10.Pia kampuni hiyo
imetoa vifaa mbalimbali vya kusomea kwa shule hiyo ambayo pia inatoa elimu kwa
watoto wenye ulemavu wa akili.
Msaada huo umetolewa kupitia
taasisi isiyo ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust,nayo ya jijini Dar es Salaam
ambayo imekuwa ikijishughulisha na kuboresha mazingira ya watoto kusomea kwa
kutoa misaada ya madawati na vifaa vya kusomea mashuleni ikiwemo vitabu na
tangu ianzishwe tayari imetoa misaada kwa shule mbalimbali nchini.
Akiongea katika hafla ya
kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika shule ya msingi Mbuyuni Meneja wa
Mawasiliano na matangazo wa Aggrey&Clifford
Bw.Oliver Mutere alisema kuwa msaada huo ni kuunga mkono jitihada za
serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini ambayo inakabiliwa na
changamoto mbalimbali.
“Kampuni yetu ambayo ina
mtamdao katika ukanda wa Afrika Mashariki na ikiwa imeajiri wataalamu wa Nyanja
mbalimbali inajua umuhimu wa elimu bora na ndio maana tumetoa msaada huu
kuwawezesha watoto hawa wasome katika mazingira mazuri ili waje kuwa wataalamu
wazuri katika siku zijazo na tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuboresha
elimu nchini”.Alisema.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi
Hassan Maajar Trust ZenaTenga, alisema
ana imani kuwa msaada huu utawanufaisha wanafunzi wengi katika shule ya Mbuyuni
watakaotumia madawati haya “Mazingira bora ya kusomea ni jambo la muhimu katika
kuboresha elimu nchini na huwezi kuongelea elimu bora wakati watoto wanasoma
wakiwa wamekaa sakafuni”.Alisema na kutoa wito kwa makampuni na taasisi zingine
kulivalia njuga tatizo la upungufu wa madawati mashuleni na kulimaliza kabisa.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu
wa Shule ya Mbuyuni Dorothy Malecela alishukuru kwa msaada huo ambaye shule
yake imepata na alitoa wito kwa wafadhili wengine kuendelea kujitokeza kusaidia
jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo
katika ufanikishaji wa kutoa elimu bora.
0 comments:
Post a Comment