Nafasi Ya Matangazo

August 10, 2015

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Anthony Mavunde akikabidhi kombe kwa Mabingwa wa Michuano ya DC Cup 2015 timu ya Kanisani FC baada ya kuibuka na ushibdi w bao 4-1 dhidi ya Ilolo FC katika fainali zilizofanyika jana katika uwanja wa Shule ya Msingi Chanzugwa.

Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa jana yalifikia kileleni katika viwanja vya shule ya Msingi Chazungwa kwa kuzikutanisha timu za Ilolo Fc na Kanisani Fc ambapo timu ya Kanisani Fc iliibuka kidedea kwa ushindi wa goli 4 dhidi ya bao 1 la wapinzani wao.

Mgeni Rasmi wa mashindano hayo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Nd Anthony Mavunde ambaye pia ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo.

Wakati akifunga mashindano hayo,Mkuu wa wilaya amezitaka timu zote zilizoshiriki katika mashindano hayo kuunda vikundi vya uzalishaji mali na visajiliwe rasmi ili kuanza mchakato wa upatikanaji wa mikopo na mitaji ya kufanyia shughuli za kiuchumi. 
 Mtanange ukiendelea.
 Mabingwa wa DC Cup 2015 Kanisani FC wakiwa katika picha ya pamoja.
 DC Mavunde akizungumza kuhusiana na mashindano hayo.
Posted by MROKI On Monday, August 10, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo