Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikata utepe
kuashiria kumkabidhi kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), msaada wa Zizi
jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa
Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha
jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence
Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa tatu kushoto), akikabidhi
Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada wa
Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango wa Airtel
‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa
Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo,
Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas
Emmanuel.
************
Fursa “Tunakuwezesha” imemkabidhi kijana Jonathan Clement
mkazi Migungani kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani
Arusha ng’ombe wawili, banda la kisasa pamoja na mafunzo ya
biashara ambayo itamsaidia kuinua biashara yake ya ufugaji na kumuongezea
kipato chake.
Jonathan kijana mwenye umri wa
miaka 21 na elimu ya kidato cha nne amekabidhiwa mtaji huo ambapo awali
alikuwa na ngomb’e wawili na banda lililochoka na alikuwa na
changamoto ya elimu ya ufugaji na madawa ya mifugo.
Jonathan
ameishukuru kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa kumpatia msaada huo
amesema “biashara yangu ya ufugaji sasa itapiga hatua. Naamini miaka
michache ijayo nitakuwa na mifugo mingi sana na soko langu la maziwa litakuwa
kwa kasi. Na vile vile itaniwezesha kuinua familia na biashara yangu kwa
ujumla”.
“Hii ni
bahati ya peke kwangu kutoka Airtel, kwani ni vijana wengi sana wanatamani
kupata hivi nilivyovipata lakini hawakupata bahati hii. Nawahimiza vijana
wengine wasikate tamaa na wajitokeze kwa wingi kwani Airtel Fursa ipo
kutuwezesha vijana”.
Akizungumza baada ya
makabidhiano, Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, alisema
“mpango huu ulibuniwa ili kuwawezesha vijana na kuwakwamua kiuchumi. Jonathan
amepitia changamoto nyingi kufikia hapa alipo alianza na ngombe wa kukopeshwa
kutoka kwa mjomba wake kwa makubaliano kwamba atakapopata ndama wa kwanza
atakuwa wa kwake. Lakini leo hii tumemuwezesha kuwa na jumla ya ng’ombe watatu kwenye zizi lake”.
“Airtel
kupitia mradi wake wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” imempatia msaada huu
Jonathan baada yakuridhishwa na hatua ya ufugaji pamoja na kuonyesha nia yakuwa
mfugaji bora hapa nchini” alisema.
Bayumi aliwataka vijana
wachangamkie fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huu unawalenga vijana wenye
umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza
kutimiza malengo yao..
“Program hii inahusisha vijana
kutoka sehemu mbalimbali nchini alisema.
Ili kijana kushiriki au
kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma
ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
Jina, Umri, aina ya biashara na
eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com< mailto:airtelfursa@tz.airtel. com>.
ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu
program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com<
0 comments:
Post a Comment